Hans Poppe aunga mkono kutafutwa Kocha mpya Simba SC, asema timu haijawa na muunganiko mzuri

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe, amerejea nchini na kuvunja ukimya akianza na suala la nafasi ya Kocha Mkuu wa Simba inayoshikiliwa na raia wa Cameron, Joseph Omog.

Omog amekuwa katika mjadala huku wengi wakiamini ana nafasi ndogo ya kubaki Simba baada ya kuwa na taarifa kuwa uongozi unaonekana kutoridhishwa naye, na umeanza kusaka kocha mpya kimyakimya.

Katika mahojiano na Championi Jumatano, Hans Poppe amesema kwa kuwa alikuwa nje ya nchi, hakuwa ameshiriki mambo mengi ya Simba lakini haoni kama kuna ubaya Simba ikiamua kubadili kocha.

"Kama inawezekana kubadili kocha kwa ajili ya kupata matokeo sioni vibaya. Kocha anaajiriwa kwa ajili ya kusaidia kupatikana kwa matokeo bora.

"Kama kocha atakuwa ana matokeo mabaya au yasiyoridhisha, sioni kama kuna ubaya kumbadilisha eti kwa sababu ya hofu", alisema.

Alisema uongozi unapaswa kupima na kuangalia kwa kuwa suala hilo si katika kitengo chake na kama unaona inawezekana kubaki naye, au kubadilisha mambo kwa nia njema, yote ni mambo sahihi.

Kuhusiana na kikosi cha Simba kinavyocheza hadi kilipo sasa, Hans Poppe ambaye hapendi kumung'unya maneno amesema;

"Hatuna mwendelezo mzuri katika kikosi chetu. Leo unashinda saba kesho sare, nafikiri kuna tatizo la kufanyiwa kazi. Bado timu haijawa na muunganiko mzuri.

"Sasa hili ni jukumu la bechi la ufundi kutengeneza kikosi ambacho kinafanya vizuri katika kila idara".

Simba inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi tano na kushinda tatu huku ikiwa imetoa sare mbili.

Kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusiana na Omog kubaki au kuendelea huku baadhi ya mashabiki wa Simba wakitaka aondolewe.

Lakini wajuzi wa mambo ya soka wamekuwa wakisisitiza kuwa bado mapema kwa kocha mwenye kikosi kipana kupata uhakika wa mambo na Simba wanapaswa kuwa wavumilivu angalau kwa mechi tano zijazo.

Tayari imepachika mabao 14 na kuruhusu matatu katika mechi hizo tano.

Chanzo: Championi
 
Mpeni nafasi zaidi, ligi ndio inaanza.
Haelekei kuwa na mafanikio mbeleni kwa hivyo heri kuamua mapema.

Naunga mkono hoja ya Hans Poppe, unasajili kwa gharama kwa kutarajia kupata matokeo mazuri uwanjani. Ijapokuwa mpira una matokeo matatu ambayo huwezi kuyaepuka lakini si kama tulivyotarajia Wanamsimbazi
 
Soka la Bongo ni pasua kichwa.

Tuwaache wafu wazike wafu wao.
 
Kwa kauli hiyo ya makofia, safari ya Omog imeiva. Ni suala la muda tu. Nikiwa mwana Yanga, napenda hili litokee haraka ili wajivuruge wenyewe. Kocha mpya atahitaji kuwajua wachezaji na kujipanga upya kwa formation yake. Hayo yote yatakuwa na gharama zake uwanjani.
 
Mwaka huu pande zote zina Makocha wabovu. Unaombea Simba mvurugano ilhali wewe hauko salama kwa Lwandamina. Hujasikia kila siku mashabiki wakilalamika kuhusu kocha wa Yanga?

Tuna amini kuwa suluhisho kwa sasa Simba ni Kocha mpya.
 
Yes Lwandamina analalamikiwa. Kwa hiyo kuna reason ya kufanya mabadiliko. Lakini Simba mnataka kutengeneza gari linatembea vizuri. Do not fix it, if not broken!
 
Simba bwana kwa hiyo wanabadilisha kocha ili wapate matokeo mazuri kila siku..kwenye soka hamnaga hicho kitu..Timu kubwa zinabadilisha makocha na bado zinafungwa..Wasijidanganye..hata wakimtimua Omog kufungwa kupo palepale, soka halina mwenyewe
 
Matokeo matatu ya mpira uwanjani hayaepukiki. Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa timu haijawa na muunganiko mzuri.
 
kule Anfield tushaanza kupiga jaramba la [HASHTAG]#kloppout[/HASHTAG] .

na Msimbazi nako walianzishe [HASHTAG]#omogout[/HASHTAG] !
 
kule Anfield tushaanza kupiga jaramba la [HASHTAG]#kloppout[/HASHTAG] .

na Msimbazi nako walianzishe [HASHTAG]#omogout[/HASHTAG] !
Na kule kwa washika mitutu (Arsenal) wao hawana mageuzi. Au ameamua kukita kambi mpaka mwisho kama Mugabe?
 
Matokeo matatu ya mpira uwanjani hayaepukiki. Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa timu haijawa na muunganiko mzuri.
kama haijawa na muunganiko mzuri kubadilisha kocha ndio suluhisho la kudumu?
 
kama haijawa na muunganiko mzuri kubadilisha kocha ndio suluhisho la kudumu?
Exactly.. Kocha ndo anayeunganisha wachezaji kulingana na mfumo anaofundisha. Kwa vile baada ya msimu kwisha ripoti yake ilifanyiwa kazi kutokana na upungufu ulijitokeza.

Sasa kwanini mambo ni yale yale tu? Lipo tatizo
 
haya kazi kwenu ila mkikosa ubingwa msitafute mchawi nani
 
Watu wanataka kupiga ten percent ya kocha mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…