Hans van Pluijm Mfano wa kocha wa Kuigwa..

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Kocha wa Yanga raia wa kiholanzi ila sasa ikiishi Ghana ni mfano wa kocha wa kuigwa na makocha wetu wazawa.

Amewai fundisha timu mbalimbali kwao Holland,Ghana Uarabuni na Sasa akiwa Yanga,Akiwa kama mkocha mkuu wa Yanga amefanikiwa kuipa Yanga vikombe vya ubingwa na Vodacom na pia kuingiza timu hatua za makundi kombe la shirikisho.

Kocha uyu amefanikiwa kubadilisha uchezaji wa timu ya Yanga kutoka matumizi ya Pasi ndefu mpaka timu kucheza pasi fupi fupi na kupanga mashambulizi yenye nguvu.

Leo Yanga imecheza na Kagera Sugar na kushinda jumla goli 6 kwa 2 za Kagera sugar,Wafungaji akiwa ni Pamoja na Obrey Chirwa mchezaji wa zamani wa Platinum fc ya zimbabwe.

Kabla ya hapo watu waliponda sana usajili wa kijana Chirwa kwan alisajiliwa kwa pesa nyingi tu ila Hans Van pluijm akasema kijana yuko safi niachieni nitamtengeneza leo naona wote waliokua wanamponda vichwa chini,leo kachapa goli mbili jumla atakua na goli 4 kama maktaba yangu iko vizuri

Pia Hans var der Pluijm alimleta Mkongwe Vicent Bossou raia wa Togo watu wakaponda sana ila leo amekua kati ya beki tegemeo wa Yanga na timu yake ya Taifa/Togo akiwa amesaidia kufuzu kombe la mataifa huru ya Afrika.

Hakika hans var der pluijm hongera nani mfano bora wa kocha wa kuigwa.

Sitashangaa kama utashinda tuzo ya kocha bora mtawalia msimu huu kwani unastahili.

Hongereni Yanga kwa Ushindi wa leo.
 
We jamaa umeridhika kabisa?
Malengo ya yanga,,simba na azam ni kuleta ubingwa wa Afrika hapa nyumbani.
Hans kashindwa ktk hilo...Makundi yanga kaingia kupitia kwa kibonde na kaishia kuwa mwa mwisho.
Mi napenda tim zetu zifike mbali hivyo kwa yanga naona Hans kafika mwisho...Aje huyo Mzambia
 
Kocha bora unafungwa na muunganiko wa wapiga debe wa stand?
Mtani bana Muunganiko wa wapiga debe siyo Vp wewe kama misimu miwili ivi hao wapiga debe walikufanyaje pale Kambarage??

Usitukane mamba kabla hujavuka mto,mfunge kwanza toto kesho halafu ndo urudi hapa.

Ref matokeo ya 22 feb 2015 Stand united vs Simba halafu mwenyewe uje utupe mrejesho apa.
 
Unajua mara ya mwisho Taifa stars kufuzu Mataifa huru ya Afrika?

Na unajua mara ya mwisho Yanga kucheza hatua za makundi?

Mpira ni long term investment ndugu hata Tp mazembe walianza mbali sana mpaka leo wanacheza fainali mbalimbali.

Ulikua unajua malengo ya Yanga kwenye Kombe la mabingwa Afrika/Shirikisho?

Kweli ulitegemea Yanga itabeba kombe?

Hans var der Pluijm kaifanyia mengi Yanga unakumbuka mpira wa Dusan Kondic/papic?
 
Kocha bora omog kaipeleka azam ligi ya mabingwa
Omog c kafukuzwa Azam baada ya kushinda 2 Chamanzi na kwenda Sudan kachapwa 3 kama maktaba iko vizuri dhidi ya el Merreick
 
Kikubwa pia ni falsafa ya uongozi. Kumpa muda kocha na kuwapa muda wachezaji. Ingekuwa wang'oa viti, Bossou na Chirwa wasingekuwepo leo.
Moja ya chanzo cha mafanikio Yanga ni kutomuingilia kocha kwenye kazi yake. Usajili na upangaji time.
 
Kikubwa ni ligi ya VPL Tanzania kupata matokeo ya timu kuanza kushinda kwa magoli mengi maana ukame wa goli nyingi ktk mechi za ligi unaakisi ubutu wa wafungaji na kufanya timu zetu wawakilishi wetu kimataifa kushindwa kufanya vizuri.
 
Mkuu,,kwa mawazo yako hayo Tanzania tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu.
Kwahiyo unataka kunambia kuwa malengo yalikuwa kushika nafasi ya mwisho kwenye kundi?
Ni ubunifu upi Hans aliufanya ktk hatua ya makundi ktk mechi zake?
Na uhakika unajua kilichotokea Man City baada uwekezaji mkubwa wa mwarabu....sasa sijui unataka vilabu vyetu vichukue mda gani ili vifanye vizuri Kimataifa
 
Acheni kujidanganya Watanzania mpira hauna shortcut lazima ufwate mifumo sahihi yote ya mpira ndo ufanikiwe

Unajua Iceland wamewekeza kwa miaka mingapi mpaka anakuja kumfunga Uingereza?

Hawa kina Sigurdson/Gunarson wametafutwa ndugu

Iceland anapeleka wachezaji wake Kwenye academy za soka za uingereza wakajifunze mpira ndo maana leo anakula matunda yake

Mancity imenunuliwa na Abu dhabi company 2008 msimu wa kwanza anashika nafasi ya kumi baada ya kumnunua Robihno kwa dau kubwa

2009 anashika nafasi ya 5 akiwanunua adebayor,kolo toure,Lescot...nk

Azam imechukua miaka mingapi kubeba kombe la Tanzania

Umeona Serengeti boys kitu wamefanya wamepita kwenye mifumo sahihi ya soka.

Tuwe na mipango mirefu ya soka nasi tutafanikiwa
 
Malengo ya Yanga yalikua ni kuingia hatua za makundi.

Tena wamepata na ushindi dhidi ya mo bejaija.

Miaka mingne walikua wanakula hata goli sita wanatoka bila ushindi wwte
 
plujimu anashindwa hata na kocha wa stand united
 
Hahaha unajua ukitaka kuwa shabiki wa Simba au Yanga ni lazima ujitoe ufahamu kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…