Haonga aombe radhi kwa upotoshaji kodi za Mbolea; Rais amesema Corona ndo chanzo cha kupanda bei ya Mbolea

Haonga aombe radhi kwa upotoshaji kodi za Mbolea; Rais amesema Corona ndo chanzo cha kupanda bei ya Mbolea

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Leo wakati wa hotuba yake baada ya kuapisha mabalozi Mh Rais alijaribu kuhusiana na kupanda kwa bei ya mbolea nchini , jambo ambalo linaonekana wazi kuwa litaleta athari sana katika suala letu la chakula hapo mwakani. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kupanda kwa bei ya mbolea nchini kumetokana na uzalishaji mdogo wa bidhaa hiyo katika viwanda vya nje ya nchi kufuatia kufungwa na kupunguza uzalishaji baada ya ugonjwa wa Corona.

Lakini hapo nyuma tuliona jinsi aliyekuwa Mbunge wa Mbozi Pascal Haonga akituambia kuwa Serikali imepandisha Kodi ya Mbolea na kupelekea Malalamiko kadhaa zikiwemo threads zilizoshushwa humu Jamvini.

Mheshimiwa Haonga alisema:
"Serikali ya C.C.M itaua kilimo,imepandisha kodi ya pembejeo za kilimo ili kukomoa wakulima mbolea ya kupandia mazao aina ya DAP imeongezeka bei kutoka 52,000= hadi 92,000/=.Mbolea za kukuzia Mf.UREA kutoka 48,000/=na sasa ni 80,000/= na CAN kutoka 40,000-60,000/=."

Kama hilo si sahihi Mh.Haonga alipaswa akanushe hilo na aombe radhi kwa upotoshaji huu unaoweza kuleta chuki kwa wananchi hususan wakulima kwa serikali yao. Hili inaonekana alizusha mno na kwa nafasi yake kama mtunga Sheria aliyepita alikuwa na uwezo wa kureserch na kuthibitisha hiyo taarifa yake kwanza kabla ya kuisambaza. Haonga alikwenda mbali zaidi na kuweka hili neno "ILI KUKOMOA WAKULIMA"



 
Back
Top Bottom