Hapa ajali ikitokea nani alaumiwe?

Hapa ajali ikitokea nani alaumiwe?

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Posts
10,955
Reaction score
4,656
Jamani hizi kampeni sasa zimepitiliza!
Sasa hadi mambo ya usalama hayazingatiwi.

2i22k4.jpg
 
Jamani hizi kampeni sasa zimepitiliza!
Sasa hadi mambo ya usalama hayazingatiwi.

2i22k4.jpg

Jaribu kubandika hapo ya kwako uone jinsi Kinana atakavyokuitia Press Conference na kukuweka pingamizi kwa Tendwa
 
Alaumiwe huyo mgombea!:becky::becky::becky: Kwani anapendwa kupita kiasi
 
Ni ishara kuwa mwanasiasa huyo hataheshimu taaluma za watu na chama chake kinaona ni sawa tu. Viongozi makini wanalinda usalama wa watu na viongozi wasiomakini ni potential problem creators.
 
Actually she is a lot more better looking than the road sign.
 
Ingekuwa chama cha upinzani tungesikia wamekiuka maadili ya uchaguzi. CCM wababe wanaweza wakaweka advert hadi kwenye traffic lights na hakuna wa kuwanyooshea kidole. Aiseeee
 
Ndio Tanzania wakati wa kampeni hata vyombo vya usalama navyo vinafanya kampeni! What hell is this
 
tuendelee kuiombea hii nchi maana ni hatari tupu..
 
Aliyebandika hapo ana akili nusu, ya kutambua watumia barabara wote wataangalia alama hiyo na kupata ujumbe; nusu yake iliyopungua ni kwamba ni kusababisha ajali na pia si watumia barabara wote uangalia alama hizo za barabarani mbali na taa za kuongozea magari!!!!!!! Huo ni ujumbe tosha kuwa CCM haitambui maslahi ya wananchi wa Tanzania.
 
Umaskini wa watanzania ni vigumu kuisha mbadikaji nadhani hana hata uhakika wa kuishi!!!!!
 
Yaani kwa kweli ni kama hatuna sheria za barabarani.
 
Jamani hizi kampeni sasa zimepitiliza!
Sasa hadi mambo ya usalama hayazingatiwi.

2i22k4.jpg

Mdaiwa wa kwanza A kizigha, mdaiwa wa pili CCM, mdaiwa wa tatu tume ya uchaguzi, mdaiwa wa nne halmashauri ya jiji kwa kuruhusu ( by implication ) kuzibwa hiyo alama, mdaiwa wa tano dereva na mdaiwa wa sita mwenye gari.
 
Jaribu kubandika hapo ya kwako uone jinsi Kinana atakavyokuitia Press Conference na kukuweka pingamizi kwa Tendwa

Sidhani kama aliyebandika hilo tangazo hapo ndio maoelezo aliyopewa hiyo haina tofauti na pale unapokuta watu wanatupa takataka sehemu ambayo kuna bango "USITUPE TAKA TAKA HAPA" au unakula jojo na kutupa karatasi chini kwa mawazo kwamba wapo wenye kazi ya kufanya usafi. Tatizo la watanzania tunaamini serikali ndo itufundishe ustaarabu. Sielewi ni kwanini limeonekana hilo tu au kwa sababu ni uchaguzi, kuna mabo mengi watu wanafanya unajiuliza kama ni akili au matope yanatumika.
 
Kwa hilo hata siwalaumu CCM maana magazeti yao mmeacha kuyanunua ,television zao mmeacha kuzitazama ,wakiwaita kwenye kampeni zao hamuendi mpaka mlazimishwe kufunga biashara na wengine wasafirishwe kwa malori kila wanalosema mnawajibu HATUDANGANYIKI sasa wafanyeje zaidi ya kutafuta mahala ambapo wana uhakika kuwa lazima mtapaangalia.Lakini hii imezidi inabidi vyombo vya kulinda sheria viingilie.
 
Back
Top Bottom