Hapa kuna mapenzi kweli?

Sioni kama kuna ubaya. Kila mtu na matakwa yake.
Bora huyo aliyedai hataki mwalimu, kuna mmoja anadai hawezi kuoa mwanamke mwenye miguu myembamba.
Watu sahivi wana vigezo kibao ila kuchamba kwingi wataondoka na kinyesi.
 
Kama wanaume wanavyosema mke mzuri ni mwalimu naye ana haki ya kuchagua mume anayemuona ni mzuri. Tuwe wakweli hivi waweza mpenda msukuma mkokoteni kisa handsome; yani kama ule mziki wa zali la mentali. Hamna kitu kila mtu ana malengo hata kwenye mapenzi tusizugane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…