HAPA LAZIMA UKIMBIE

mnzagila

Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
69
Reaction score
40
Nilikutana na mshikaji wangu Tandika stendi ya mbagara, akanistua kwa nyuma akisema "malogy mathematic ndio wew? upo kaka?". Nikamjibu nipo k iongozi tunasindikiza wenye maisha yao, akacheka sana,, Mara akaanza kuzungumilzia matatizo ya familia yake, nikamwambia tuyaache hayo mim mwenzako nimepitia makubwa, aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake, NIKAMSTOPISHA nikamwambia " Unadhani familia yako ina matatizo?" Basi sikiliza kisa changu hiki….
"Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu, mimi na huyo mjane tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu ambae alikuwa mkiwa baada ya kufiwa na mama kitambo tu akaamua kumuoa binti yangu wa kambo (yaani binti wa huyu mke wangu niliyemwoa akiwa mjane), hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake.
Baadaye binti ya mke wangu yaani binti yangu wa kambo (ambaye kwa sasa ndiye mke wa baba yangu na hivyo kuwa pia mama yangu wa kambo) alipata mtoto wa kiume. Mtoto huyo wa kiume akawa mdogo wangu kwa sababu tulichangia baba mmoja. lakini kwa vile pia alikua ni mtoto wa binti wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake huyo mdogo wangu.
Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana (yaani binti ya mke wangu ambaye pia ni mke wa baba yangu) ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake na mwanangu (mwee!!). Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kuwa shemeji wa mtoto wangu (achilia kuwa babu yake!!) ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wa binti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe.
Kabla sijammalizia jamaa akaondoka
Mimi sio mtu wa mchezomchezo
Sipendagi Ujinga
 
hii ndio jf bwana ukiwa na vistress uchwara vinaisha[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Hakuomba panadol? Maana mi kichwa kingeuma kwa kweli ingawa ningependa kuendelea kusikiliza na kujua mko kijiji gani
 
kwani hayo ni matatizo ya familia? Baba yako aliyataka na alijua hilo, wewe endelea na maisha tu
 
Ahaaaaa nimecheka mpaka machozi yametoka da!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Huo ni zaidi ya undugu yan utaifa kabisa
 
Kweli wewe sio mtu wa hovyo hovyo.. hivyo hutaki kusikia vitu vya hovyo hovyo kwa watu hovyoo hovyoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…