Hapa mada pia hugeuka makapi, huchacha....

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kipya kinyemi waswahili walisema.... Lakini upya haudumu.... Labda kisitumike... Na kikikaa sana bila kutumika huchacha kwa vile vinavyochacha... Huharibika kwa vile vinavyoharibika na hufikia kikomo cha matumizi kwa vile vyenye ukomo... Vingine huisha fasheni....
Unapoingia JF na kukutana na NEW POST fasta utaangalia ni maudhui gani na kama yanakuvutia kuchangia utachangia... Kadiri NEW POST inavyochangiwa na watu wengi ndio kadiri inavyokamuliwa maudhui yake na taratibu huwashibisha wachangiaji na mwishoni kubaki kama makapi tuuu.. Hapo Inakuwa haina nguvu ya kuchangiwa tena...
Ukiona kuna post ilishakuwa makapi na ni ya kitambo.. Ukiifufudua haiwi mpya tena bali ni sawa na kupasha kiporo ama kui recycle.. Lakini kuna post zina roho.. Kuna post zinaishi.. Maudhui yake hayachuji... Maana yake hubaki ile ile jana leo na kesho
Ila bwana kuna post zinachacha.. Na zinachacha vibaya kweli... Ndugu yangu ukiona post yako imechacha usikate tamaa utaandika nyingine alhamdullilah itafanya vema... Itanoga kama chakula kitamu kilichopikwa na mwanamke wa kitanga... Usiwe hatee mpaka unajulikana kwa post za wengine... Ufundi haufanani
 
Safii, kama naziona post za mtemi DEOGRATIUS NALIMI KISANDU zinavoish kitoto kwa kudunda utosi[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hapa umezungumzia nyuzi za forex na uzi wa Field Marshal ES
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…