Twende taratibu huenda tukaelewana vizuri!Safi kabisa, kwanza nakutoa wasi wasi ya kuwa uhalisia hata wewe ukiutaka unauona, yaani upo, mfano wa uhalisia ni kuwepo wewe, na kuwepo kwa jua na usiku na mchana na kuwepo kwa njaa na mfano wake, huu wote ni uhalisia.
Kwanza kabisa, ni nini maana ya Elimu ? Elimu ni kukidiriki kitu kama kilivyo, yaani kiwe kweli na si kinyume chake.
Ushahidi ni kuwa hakuna mtu aliye buni namba fulani, kwamba namna moja ameibuni fulani, na namba mbili ameibuni fulani, zaidi ya kutoa majina.
Pili, hakuna muanzilishi wa elimu fulani bali wapo walioweka kanuni juu ya elimu fulani, sababu namba zilikuwepo hata kabla ya hao walio weka maana zao juu ya namba walizo zikuta.
Ushahidi upo katika maana ya Dark Energy, husemwa yafuatayo juu ya maana ya Dark Energy.
Nanukuu :
1. Dark Energy is a theoretical form of energy postulated to act in opposition to gravity and to occupy the entire universe, accounting for most of the energy in it and causing its expansion to accelerate.
2. In physical cosmology and astronomy, dark energy is a term that describes an unknown form of energy that affects the universe on the largest scales. (Wikipedia)
Sasa mimi sijaona jaribio lolote lililo fanywa na wanasayansi likagundua uwepo wa Dark Energy, kama lipo hilo jaribio, niambieni na mtuambie walitumia njia gani za Kisayansi kujua hil,hili swali nimeliuliza zaidi ya mara mbili humu.
Uhalisia nikuwa hakuna kiumbe kinachoweza kuumba kiumbe kingine, sababu jambo la Roho liko nje ya uwezo wa mwanadamu. Na kinyume chake ni ukweli, sababu hakuna anae weza kurudisha kiumne kilicho kufa.
Kuna Prof mmoja, aliwahi kusema anaweza kuumba "Funza" alicho kifanya, ni kuchukua mkate na mchuzi fulani, akaviweka sehemu baada ua siku kadhaa funza wakaanza kutokea, kisha akarudi darasani akawaonyesha wanafunzi wake kisha akasema ameumba "Funza" wanafunzi wake wakacheka sana.
1. Kiumbe ni nini? Unamaanisha kiumbe hai au kisicho hai?
2. Je, mimea ni sehemu ya viumbe? Hakuna mimea imetengenezwa maabara leo? Namaanisha mimea kama michungwa, papai, mbegu za mahindi nk. Hapa tuwaulize watu wa maabara ya SUA huenda wakatusaidia
3. Huwa nasikia watu wanasema kuna wanyama na jamii ya ndege wa kisasa! Mfano, nasikia kuna kuku wa kisasa ambao ni tofauti kabisa na kuku wa kule kijijini kwetu! Hali kadhalika naskia kuna ng'ombe wa kisasa, mbuzi na wanyama wengine! Hawa wametokea wapi? Maana naskia sikia chanzo chake ni maabara za kisayansi! Watu wa SUA watusaidie tena hapa
4. Watu wa Taasisi ya Afya Ifakara pia watusaidie hapa, hivi mbu ni kiumbe au sio kiumbe!? Na kama ni kiumbe, hivi haijawahi kutokea wataalamu wa maabara kuzalisha mbu kwa lengo la kutokomeza hawa mbu aina ya "anofrensi" wanaotuletea malaria? Au ni habari za uzushi hizi maana mwenzetu unatwambia hakuna mwenye uwezo wa kutengeneza kiumbe
Labda nimemezeshwa taarifa za vijiweni, hebu nitoe tongotongo kwa haya nayoyasikia sikia ili niongeze ufahamu na Mimi
Na jambo jingine ni hili nalotaka Msaada wa ufahamu toka kwako:-
1. Kwa kuwa hakuna aliyebuni namba kwa maana zilikuwepo, yaani binadamu wamezipa majina tu, Je, hakuna uwezekano binadamu hao waliozipa majina namba kuzitumia namba hizo hizo kwa namna watakavyo wao kwa lengo la kuwasiliana wao kwa wao na kuficha taarifa hizo kwa watu wengine!?
2. Pili, umesema hakuna aliyeanzisha elimu bali wapo walioweka kanuni zao kwenye hiyo elimu.
Swali ni Je, hakuna uwezekano katika kanuni hizo unazodai wameweka ndio code zenyewe za walichokilenga!? Yaani walificha taarifa fulani kwa kundi fulani katika kanuni hizo?
Hapa najaribu kwenda na wewe taratibu huenda nikakuelewa au wewe ukaelewa wanachojadili wadau humu
Sent using Jamii Forums mobile app