Hapa Nape Anamaanisha Nini? Kwamba Membe Aliandika Mambo Mazito Sana au?

Hapa Nape Anamaanisha Nini? Kwamba Membe Aliandika Mambo Mazito Sana au?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema katika kitabu cha historia ya maisha ya Membe alichokiandika mwenyewe enzi za uhai wake huenda kuna sehemu kitawakwaza watu hivyo anaomba samahani kwa niaba ya marehemu.

Nape ameyasema hayo wakati akitoa salamu za familia katika hafla ya kitaifa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.

“Uandishi wa kitabu hiki yawezekana kulikuwa na mahala utakwazika hapa na pale, inawezekana wakati wa kukisoma kitabu si wote wakakifurahia hivyo kwa niaba ya familia niwaombe mumsamehe ili apate kupumzika kwa Amani,”amesema.
 
Palipokuwa na kukanyagana basi nachukua nafasi hii kumuombea msamaha Marehemu Membe ili akapumzike kwa amani.
 
Palipokuwa na kukanyagana basi nachukua nafasi hii kumuombea msamaha Marehemu Membe ili akapumzike kwa amani.
Watesi wake wanatamani kufungua midomo yao ili kuomba radhi lakini mioyo yao inawaka moto
 
Vijana wa hovyo wanasema hivi, tunaanzia pale pale tulipoishia.[emoji23]
 
Palipokuwa na kukanyagana basi nachukua nafasi hii kumuombea msamaha Marehemu Membe ili akapumzike kwa amani.
Mleta uzi sio muelewa.
Nape alimaanisha kuwa kwa wale waliowahi kukosewa na Membe akiwa hai wamsamehe.
 
Back
Top Bottom