Hapa ndipo ulipo utimilifu wa kifo!

Hapa ndipo ulipo utimilifu wa kifo!

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Utimilifu wa kifo umebebwa hasa kwenye;

MUUNDO WA MWILI.
Mwili wa kiumbe hai unatimiza kifo kwa kuwa unaweza kuugua, kudhurika na sumu, kuungua, ulaini uliopo kwenye mwili,kwenye hili naomba nieleweke hivi,mwili(hasa wa binadamu) ni laini hivyo ni virahisi kudhurika.

Kuruhusu kushambuliwa na bacteria au virus, yapo mengi lakini naomba niishie hayo tu.

Kwa binadamu jambo hili la utimilifu wa kifo linaweza kuonekana kama udhaifu,lkn kwenye mazingira ni utimilifu wa balance of nature!.

Ili kuweze kuwa na kifo ndo maana muundo wa mwili unakuwa na hayo ambayo yanaleta utimilifu wa kifo.

Kupambana na magonjwa,ajali n.k ndio inaonekana njia ya kuzuia kifo lkn binafsi sidhani cha kudili nacho ni muundo huo kuubadili!

Kama binadamu atataka kudhibiti kifo lazima adili na hayo mambo,
Pia atafute sehemu nyengine ya kuishi kwa maana watu watakuwa wengi coz hawafi au afunge jumla uwezo wa kuzaa!

Kutokana na hayo swali la kujiuliza je, mwanadamu itamchukua muda gani kuzuia kifo?

Na kwanini kifo kizuiliwe?
 
Qur nafsih dharikal mautih.... No body can stop dearh.... NO BODY BROTHER... ¡!!!.. Kila jambo aliloliahidi ALLAH lazima litimie.... Ni kusubiri muda tuu......
 
Muasisi wa uhai alishaamua kwamba binadamu atakufa, hakuna namna binadamu atakuja na technolojia ya aina yeyote ya kupambana na kifo. Ni sawasawa na kutaka kulazimisha gari la nchi kavu liruke angani kama ndege wakati mtengenezaji wa gari amelitengeneza kwa ajili ya kusafiri nchi kavu.
 
Nini kama ikiwezekana..?
 
Vipi kama ikitokea mwanadamu akaweza utaendelea kumwamini huyo muasisi wa uhai..?
 
Mimi binafsi sioni sababu za kuogopa kifo sikuomba wala kulazimisha kuzaliwa sasa iweje niogope kufa.
 
Qur nafsih dharikal mautih.... No body can stop dearh.... NO BODY BROTHER... ¡!!!.. Kila jambo aliloliahidi ALLAH lazima litimie.... Ni kusubiri muda tuu......
Nasikia eti zaman kabla ya kutengenezwa ndege...kuna watu walibisha kabisa kama haitawezekana kutengeneza mavyuma yakaelea angani mkuu....ila sasa kila mtu ni shahidi
 
Muasisi wa uhai alishaamua kwamba binadamu atakufa, hakuna namna binadamu atakuja na technolojia ya aina yeyote ya kupambana na kifo. Ni sawasawa na kutaka kulazimisha gari la nchi kavu liruke angani kama ndege wakati mtengenezaji wa gari amelitengeneza kwa ajili ya kusafiri nchi kavu.
Mkuu usijifuungie vioo...inawezekana tukafikia happo....nadhan ndio utakuwa mwisho wa dini
 
Tatizo hawa jamaa kila kitu wanakipeleka kwenye dini.. hawashughulishi fikra zao kwa kuhofu kukufuru!
siku zote kuna mtu wa kutawala na kutawaliwa...
 
Nasikia eti zaman kabla ya kutengenezwa ndege...kuna watu walibisha kabisa kama haitawezekana kutengeneza mavyuma yakaelea angani mkuu....ila sasa kila mtu ni shahidi
Nn ndege? Sema simu. Mm huwa najiuliza hawa jamaa wanaoamini upumbavu wa Mungu ndo uwezo mdogo wa kufikiri au ndo utumwa umewaingia sana??? Maana ukitumia nafasi ndogo tu ya kufikiri unagundua mtego uliopo kwenye wizi wa uwepo wa Mungu. Au ni vile hawataki kushughulisha ubongo wao
 
Mkuu usijifuungie vioo...inawezekana tukafikia happo....nadhan ndio utakuwa mwisho wa dini

Sijifungii vioo mkuu, ila naomba tu unielewe kwamba natambua sana mchango wa sayansi na ubunifu, ila kwenye hili la kifo, bado naamini zaidi maandiko kwa sababu maelezo yake yanaendana na kinachotokea kwa maisha ya binadamu hasahasa kuhusu habari ya kifo. Sayansi yenyewe haijawahi kuongea lugha moja kuhusu uasili wa binadamu.
 
Nn ndege? Sema simu. Mm huwa najiuliza hawa jamaa wanaoamini upumbavu wa Mungu ndo uwezo mdogo wa kufikiri au ndo utumwa umewaingia sana??? Maana ukitumia nafasi ndogo tu ya kufikiri unagundua mtego uliopo kwenye wizi wa uwepo wa Mungu. Au ni vile hawataki kushughulisha ubongo wao

Ni kosa kufikiri kila anaeamini uwepo wa Mungu hashughulishi ubongo wake, inategemea lakini kwa upande wako kushughulisha ubongo unamaanisha nini. Mimi sina tatizo na Maendeleo ya technolojia na ugunduzi unaendelea, nimejikita kwenye mada husika kuhusu kifo, narudia tena, maelezo yanayotolewa kiimani kuhusu asili ya mwanadamu na kifo kiimani, inatija zaidi kuliko maelezo ya kisayansi. Endelea kushughulisha ubongo mkuu
 
wapi nimekana..?
mimi hakuna aliyeniumba so siogopi kuwaza mambo kama hayo!
utakuwa na uoga mpaka lini...

Kuwaza unaweza kuwaza chochote kadri ya uwezo wako, lakini kuwaza kwako hakubadili uhalisia wa mambo.
 
Vipi kama ikitokea mwanadamu akaweza utaendelea kumwamini huyo muasisi wa uhai..?

Mkuu kuwaza chochote sio kosa, itaendelea kua mawazo tu mkuu, Imani yangu kwa Mungu haitayumbishwa mkuu.
 
Back
Top Bottom