Hapa ndipo wakaka wanapotamani kujiua

tatizo ni kujionyesha zipo. Hivi kweli wewe unanisomesha kama nani yako? kama umenipenda na darasa la saba langu wewe nipe moyo ili nikaombe funds kwingine nisome mwenyewe. Mapenzi yako ya aina nyingi, usifikirie kunipeleka shule ndiyo utanifanya mimi nione huruma eti kwa sababu nimekusomesha.

Wanaume ebu invest kwa wadogo zenu, ndugu wa karibu, na watoto yatima labda unaweza pata thawabu, kwa mkubwa mwenzio kama mimi umekula wa chuya.Umenisomesha ndiyo, akaja mwenye kununua nyumba na gari la kifahari Range sport, why do I keep you? Nakumwaga bila huruma. inawezekana dada yako alikosa hata hela ya kumsomesha na umekaa kimya sasa una invest kwa demu, unataka huyo Mungu wako akuangalie tu ukifanya ujinga kama huo, shetani lazima avuruge. Kaeni chonjo.
 

Maumivu ya kichwa huanza pole pole. Anyway, kwa mhusika msg sent, asijesema hakuambiwa.
 

Haya mambo sio saana siku hizi wakaka wamekuwa welevu sana, wanatanguliza kakinda kwanza halafu mengine baadaye. Hapo hata demu akichomoka lakini kakinda kanachipua na uzao utaendelezwa milele na milele.

Kuna jamaa yangu aliwahi fanya makosa km hayo ya kusomecha demu baadaye wamerudi Tz akapigwa mweleka, alilia km Ngedere kakatwa mkia!

Hivyo siku hizi kila mtu mjanja ila ukienda kichwa kichwa inakula kwako.
 

Hongera sana!!!

Waambie wenzio wanaingia mkenge wa kusomesha wanawake na wasichana wakitgemea ndoa. Unamsomesha kwani wewe ni mzazi wake?

Mjue kwamba msichana akiwa shuleni, akili haiko kwenye ndoa na kadiri anavyoendelea,huwa na mawazo mapana zaidi ikiwemo aina ya mwanaume atakayetaka awe mumewe.Wewe mfadhili unaweza usiwe possible candidate au husband material.

Ukisomesha fanya kama msaada tu.Ukitaka kumuendeleza awe tayari ndani mwako kama mke halali siyo kabla ya hapo.
 
madai yao wanajua kupenda sana, mtu yupo tayari ndug zake awaache hawana elimu kisa mdada kampenda anataka awe na mke msomi, sawa hayo yote yatafanyika baada ya kuoa kama unapenda mke wako awe msomi kama wewe
 
Lizy una maakili sometimez!!
 

Ushuhuda mzuri Vumbi, mwenye masikio asikie
 

Caro umewasuta!
 
kwa hili naomba niseme hivi ukimuoa na kumsomesha then later akaja akakutosa i mean akadai talaka je utakua umefanya nn?na ukisema usitoe talaka yeye atatoa penzi nje kwa huyo ampendae huku ww akikudharau na kukuona ***** tu so kama kuibiwa unaibiwa tu no way out cha muhimu upate mke au msichana mkweli hasa lakin sio hawa wa sasa wanaojali vitu badala ya mtu.
 
sure, kama m2 anashida atakubali mambo yote hata ukimsomesha atasoma vzr tu,
kama ni mke hamna shida hiyo ni familia unasaidia familia yenu
na kama unamtarajia kumuoa baadae make ur own copy (mtoto) b4
lasivyo saidia kama unavyosaidia wa2 wengine huko barabarani haungojei fadhila
note
usiweke mtego/sababu eti ukimsomesha kwasababu labda ana shida atakupenda baadae au sababu nyingine uionayo wewe, unakajitaarishia lawama bure
good day
 
Hizo hela za kunisomeshea si bora ukagawe sadaka mimi m2 asije akanisomesha et ili aje anioe na kama wakat huo nitakua simpend itakuaje? Nitajilazimisha kuolewa naye kisa kanisomesha ?? NO!NO!
 


Nzuri kaka, iko safi. Kumsomesha mwanamke kwa minajili ya kuja kumuoa ni sawa na kupanda mbegu DECI, ukitoka unatoka ukilizwa utatamani uzaliwe upya.
 
Tangazo!!!
Namtafuta mtu wakunisomesha.
Naomba ambaye yupo tayari, kwa mapenzi mema na ya kweli ani PM plz.

Mengine, kusomeshwa nini, na wapi, tutaongea huko huko.
LD hana utani jamani, ninamaanisha.
Tafadhali.
 
Tangazo!!!
Namtafuta mtu wakunisomesha.
Naomba ambaye yupo tayari, kwa mapenzi mema na ya kweli ani PM plz.

Mengine, kusomeshwa nini, na wapi, tutaongea huko huko.
LD hana utani jamani, ninamaanisha.
Tafadhali.

najitolea kukusomea Pm zote. Mwanafunzi hutakiwi kuchoka kabla hujaanza shule. Sawa eeh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…