Wikiendi hii, mapaparazi wa mtandao huu walitua pande za Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam nyumbani kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes a.k.a Mr.Misifa. Bahati mbaya hawakuweza kumkuta lakini waliishia nje ambako walivutiwa na hali ya jiko lake pamoja na dishi la Runinga yake. Hebu cheki ilivyokuwa...
<!--ThumbBegin-->
<!--ThumbEnd-->
Huu ndio muonekano wa picha ya jiko la staa wetu Dully Sykes Handsome Boy ambaye picha yake inaonekana hapo juu
<!--ThumbBegin-->
<!--ThumbEnd-->
Hapa ni mahali anapotumia kupikia chakula chake.
<!--ThumbBegin-->
<!--ThumbEnd-->
Baada ya kula huhifadhi vyombo vyake juu ya kochi hili la mbavu za mbwa bila kuviosha ambapo nzi hufanya tafrija kwenye makombo. Hapa ni baada ya kupata kifungua kinywa.
<!--ThumbBegin-->
<!--ThumbEnd-->
Hili ndio kabati lake la kuhifadhia vifaa vyote vya jikoni.
<!--ThumbBegin-->
<!--ThumbEnd-->
Ukishangaa ya Musa utaona ya Firauni.Hili ndiyo Dish ambalo 50 Cent wa Bongo, Dully Sykes hulitumia kwenye Runinga yake, ambalo ameligeuza kamba ya kuanikia nguo.
<!--ThumbBegin-->
<!--ThumbEnd-->
Pembeni ya nyumba ameegesha mkoko (gari) wake wa maana ambao hata hivyo ulikuwa na pancha katika tairi lake la mbele upande wa kulia.
http://www.globalpublisherstz.com/
<table border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="100%"><tbody><tr><td align="left" bgcolor="#cccccc"><table border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="100%"><tbody><tr><td class="news1">
Dully, babake wagombea penzi la kibinti
</td> <td class="news1" align="right" width="150">
ijumaa wikienda</td> </tr> </tbody></table></td> </tr> <tr> <td bgcolor="#999999">
</td> </tr> <tr> <td class="morenews" align="left" bgcolor="#f3f3f3" valign="top"><!--ThumbBegin-->
<!--ThumbEnd--> Tukio hilo lililosababisha mkusanyiko wa watu wengi, lilitokea Jumatano ya Agosti 20, 2008, Magomeni Mikumi, Dar es Salaam.
Shuhuda wa soo hilo la baba na mwana alitupasha kuwa Dully na baba yake, kwa nyakati tofauti walikuwa wakijihusisha katika uhusiano wa kimapenzi na Anda 18 huyo bila wao kujua kuwa wanachangia usingizi.
Walikuwa hawajuani, sasa siku hiyo Dully katoka nyumbani kwake Tabata kwenda kumsalimia baba yake kule Magomeni, alipofika ndiyo akamkuta Mzee Abby akiwa na hicho kibinti ndipo zogo likaanza.
Dully akawa anadai yule demu ni mtu wake, pia Mzee Abby anatamba kwamba yule ni mpenzi wake. Ikafikia kipindi Mzee Abby alikasirika, akamwambia yule msichana achague mmoja kati yao, ama yeye au mwanaye wa kumzaa.
Mtu na baba yake wakataka kukunjiana ngumi, lakini wasamaria wema walimuweka Dully pembeni na kumuomba aache mambo yaishe naye akakubali, kilinena chanzo chetu kabla ya kuongeza:
Wakati Dully anabembelezwa kuachana na ugomvi, yule msichana alipata mwanya na kutokomea kusikojulikana.
Pamoja na ushuhuda wa chanzo chetu, gazeti hili lilifanya uchunguzi katika eneo lililotokea tukio na kujiridhisha kwamba ni kweli sekeseke kati ya Dully na baba yake lilitokea.
Hata hivyo, Dully alipopewa na mwandishi wetu nafasi ya kuongea, alikanusha kugombea penzi la kibinti na mzee wake: Mimi siwezi kufanya kitu kama hicho, mkiandika nakwenda mahakamani.
Aidha, katika kuonesha kwamba mtu na baba yake walipanga kamchezo ili kulizunga Ijumaa Wikienda, mwandishi wetu alipopiga namba ya simu ya mkononi ya Abby Sykes, iliita bila kupokelewa hata ilipojaribiwa zaidi ya mara 10.
Baadaye, Mzee Sykes akitumia simu ya Dully, aliongea na gazeti hili na kukanusha vikali madai hayo: Mimi sitaki muuze gazeti kwa kunidhalilisha, mkiandika hiyo habari tutafikishana mbali.
</td></tr></tbody></table>
http://www.globalpublisherstz.com/2008/09/01/dully_babake_wagombea_penzi_la_kibinti.html