Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Milio ni Mingi Wakuu!
Hapa Moja haisomi Mbili haikai. Yàani nimevurugwa kishenzi.
Harusi yàngu ni Mwezi huu. Alhamdulullah Watu wamechangachanga na tumefikia Asilimia 90% ya michango. Hapa bado nakimbizana na Suti yàngu àmbayo ñàona fundi nguo anataka kuniletea pigo za kiwaki. Mtu nimempa nguo tangu Mwezi wa sita mwanzoni nikamwambia shughuli itakuwa Mwezi wa Saba mwishoni, lakini Mpaka Leo Mwezi wa Tisa hajakamilisha. Nikipiga Mtu kûna Watu wataniona Mimi ndiye mbaya. Wakati Siku zote Mimi ni Jemadari Akudos, Taikon Master àmbaye licha ya kuwa na Mkanda mwekundu na mweusi wa mapigano ya kivita lakini sijawahi kumpiga Mtu hata Kofi Moja.
Lakini Wakati huu Kwa jinsi nionavyo hizi Hasira zangu zilivyo sijui, tuombe Mungu tuu maana nahisi kûna jambo baya linaweza kutokea. Kwanza Mimi nilipoenda nje ya nchi nikahitimu Mafunzo nilifikiri kuwa Mtu WA Kwanza nitakaye Mpa zawadi ya kimedani ya Mafunzo niliyonayo lazima atakuwa mwenye ujuzi wa mapigano, íwe Karate, Judo au hawa wacheza masumbwi. Sasa huyu fundi sijui nakuambia, sijui! Ngoja tuone
Lakini Hasira zangu zilianza kuchachamaa tangu pdf la utumishi lilivyotema. Fikiria unafungua Notes za kozi ulizosoma Miaka mitano iliyopita, NI kama unasoma kitabu kipya. Nimefungua notes za kozi nilizosoma niliishia kuzitazama na kujiuliza hivi NI Mimi ndîo nilizisoma hizi nikahitimu chuo au kûna namna zimebadilishwa. Kîla kitu ni kipya Hapa. Ninaangalia cheti na GPA niliyopata àmbayo NI second Upper Class 3.9GPA ñàona kama mzaha.
Kwa jinsi hizi notes zilivyo Wala siamini kama ndiye Mimi huyu niliye- score hii GPA.
Basi nitafanyaje, sina jinsi. Kazi naitaka Pesa naitaka. Itabidi nianze ratiba ya Kusoma. Dadeki! Mavitu hayaingii akilini. Kîla nikisoma yananidanganya kama yameingia alafu nikienda kunywa Maji nikirudi nikisema ni-revise najikuta Na-bar yàani Akili inabaa siô pouwa. Sikumbuki chochote.
Hivi nitakumbukaje Wakati Miaka yôte mitano imekuwa Miaka ha hekaheka nje ya mfumo wa kile nilichosomea.
Kazi nilizofanya Nyie! Shughuli nilizozitenda zili-erase kama siô ku-lock ma-file yôte ya Taaluma yàngu.
Hapa ni kama nimevurugwa ingawaje Watu wakiniona nikivaa Mkanda nje hudhani mambo yàngu yapo Sawa. Kumbe!
Nitoe background kidôgo ya Maisha niliyopitia baàda ya kumaliza chuo Miaka mitano iliyopita;
1. Nilianza kwa kujitolea
Nilijitolea mpaka nikakoma. Waliniambia nijitolee alafu nitapamo Ajira humo, thubutu Yake Ajira zikitoka wanapewa Wengine. Kumbuka sipewi hata Mia. Huyo nikasema ngoja niende kujitolea serikali kwani nilisikia watakaojitolea watapewa kipaombele.
Huyo nako Huko nikafanya wee Mpaka Soli za Viatu vikapinda upande mmoja. Jàmani nilitia huruma. Jàmani ungeniona nilivyopauka, kama Muha mtembeza Vyombo.
Mademu walinikimbia kama mgonjwa wa Ukoma. Nilikuwa napiga pass ndefu kama za bundesiliga.
Kûna Siku nakumbuka natoka zangu Kazini na Wala siô Kazini Kwa sababu sikuwa nalipwa, sijui niite kibaruani labda utumwani au Sobibo , Siku Ile Njaa iliniweza Aiseeh!
Nilijikuta napiga Yowe Njiani Uuuuuwwiiii! Watu wakawa wananishangaa, Mimi mwenyewe nikawa najishangaa imekuwaje tenà, sijui ilikuwaje nikapiga Yowe. Nafikiri mafaili kichwani yalisokotana Kwa sababu ya Njaa Sasa Wakati nadhani Nawaza kuwa napiga Yowe mawazoni kumbe napiga laivulaivu na Nipo mubashara.
Wapita njia walikuwa wakanitazama huku Wengine wakinipimishia na kunilinganisha na Vichaa. Kîla aliyenitazama na macho yake yakafika kwèñye Viatu vyangu, alihitimisha kuwa Mimi NI aidha chizi Fresh yàani kichaa àmbaye kinaanza, Wengine waliniona kama chizi profess kutokana na jinsi nilivyovalia mkandanje na nywele Ambazo hazivutii Sana.
Wengine wakawa wananidhihaki, wakisema kûna Watu hasa ndugu zangu wamenitoa kafara ili Wapate Utajiri.
Moyoni nikaguna. Mmmh! Imefika nafananishwa na mandondocha. Kwèli ninakolekea siko.
Huyo Kwa aibu huku fedheha ikinifuata Nyuma kama kivuli changu nikaharakisha nikiwa nimeweka Mikono mifukoni pia nikiapa sitapita tenà njia hiyo.
Nikaacha Kujitolea.
2. Nikajiingiza kwèñye Bodaboda.
Baàda ya kuona sina ujanja Sasa. Kazi Hakuna. Nikafikiria nini chakufanya. Kwa kweli kichwa ilipata Moto. Siku zaidi ya Tano sijui nini nifanye, sitaki kueleza nilipokuwa naishi, sitaki kukumbuka stress Mimi.
Nikapata wazo la kuwa dereva bodaboda. Nikaliafiki Kwa sababu kujifunza niliambiwa haitachukua Siku nyingi. Basi kweli nikajifunza bodaboda ndàni ya Siku Mbili nikajiona nime-master.
Huyo nikapewa Boda la Mkataba, Sasa kutafuta kituo cha kupaki ndîo kimbembe, kumbe kîla kituo kina Ada ya kuingia na Huwezi ingia bure. Nikapatana na wahusika WA kituo cha bodaboda kuwa kwèñye Ada ya kuingia àmbayo ni Laki Moja. Nitatoa kila Siku elfu tano Kwa Mwezi mzima àmbapo watapata Laki na hamsini wakakubali.
Boss nampa 10k Kwa Siku, kijiwe natoa 5k Kwa Siku hivyo kîla Siku itanipasa nihakikishe napata 15k ya Watu Kisha na yàngu. Bahati nzuri 10k ya boss niliambiwa nitoe kîla mwisho WA wiki hivyo Kwa wiki NI Tsh 70k.
rooo! Roooong! Raaaaaa! Piiiiii! Piiii! Hizô sauti Sasa ndîo zilianza kuingia katika kichwa changu. Zilikuwa kama wimbo wa Taífa kîla niamkapo nakuwaza wewe, nitembeapo na nilalapo zikawa zinaimba akilini mwangu. Ziliniathiri Haki ya Nani.
Usiku ndîo napiga mishe ya Pesa ndefu mpaka elfu 20 Kwa Usiku mmoja. Lakini Siku isiyo na jina ilifika. Mamaaeee Zake Yule dereva wa Lori.
Mimi natoka zangu Kibaha kumpeleka mteja, narudi zangu home kwani nimeshatosheka na siku hiyo, nikiwa pale Ubungo mataa napita nikielekea mwenge nashangaa Lori linalotokea upande wa Riverside lipo Nyuma yangu wanguwangu kama limekatika breki, najaribu kulikwepa nashangaa Bajaji hii Hapa. Dadeki, nikaivaa Bajaji paah nikarushwa Huko upande wa sheli. Kwa Bahati tuu nikajikuta ninakimbia hovyohovyo. Nafikiri nilidata.
Nikaachana na bodaboda nikasema ya nini kujifia. Tulimalizana vipi na mwenye pikipiki hiyo ni Stori ingine.
3. Nikaingia kwèñye Udalali wa viwanja, Nyumba na Magari.
Dadeki Huko nako sitaki kukumbuka. Wala sitahadithia. Kumbe vile viwanja nilivyoambiwa nividalalie vilikuwa vya kitapeli. Saa ngapi nisijikute korokoni? Dadeki! Nikaja KUTOLEWA baàda ya kukaa kama Siku tatu hivi.
4. Huyo nikaenda Morogoro kuwa Sarange(Mpiga Debe) pale Msamvu Stendi
Kuvutana na wasafiri na àmbao siô wasafiri. Aliyefundisha Ile Kazi ya usarange ungemwona alivyovalia kiafsa usingeshangaa Kwa nini nilishawishika kuingia kwèñye Kazi hiyo. Jamaa alikuwa anavaa Vizuri kuliko walioajiriwa manispaa, uvaaju wake ulikuwa Karibu Sawa na Watu wa serikali kuu. Wengine walimwona kama Afisa usalama kumbe jamaa Hana lolote. Piga Kazi! Kwanza lazima ujifunze kuongea ongea. Mimi kiasili siô mwongeaji Sana ila naandika. Lakini Kazi ya usarange ilinipa uzoefu mpya, uhusika mpya na lugha mpya.
Nikaiacha baàda ya kudokezwa Dili la dagaa wa mwanza.
5. Nikaenda Mwanza kuwa mchuuzi wa dagaa wabichu Kutoka visiwani kûja Mwaloni
Nikafanya miezi miwili, kûna Siku ziwa likachafuka Manusura nifie Majini. Nikasema ujûmbe huu nimeulewa nikaacha.
6. Nikaja Dsm kuwa Video King. Wale Wanaume wanaokuwepo kwèñye video za Muziki ya Wasanii.
Hapo nikafanya miezi mitano nikaona Hapa nikileta mchezo nitavuta Madawa au kuwa shoga. Nikakimbia.
7. Nikaenda Morogoro kiwanda cha Polister
Dadeki masaa kumi na Mbili kazikazi Mshahara wake ñàona aibu kuutaja. Yàani NI zaidi ya kidunchu alafu Kazi NI ngumu ile sijapata kuona. Nikakimbia
Nimefanya Kazi nyingi Ambazo zimenisahaulisha hata nilikuwa nasomea nini.
Sasa Siku ya usaili ndîo Siku ya Harusi yàngu.
Nachanganyikiwa Hapa. Harusi Hapa interview Kule.
Nafikiria niende kwèñye Interview na gari la bwana Harusi Likiwa limepambwa nipige usaili Kisha ndîo niende kwèñye sherehe. Bado nafikiri tuu.
Sishangai Kwa nini Vijana hawataki usaili. Hivi Kwa Kazi hizô nilizofanya au waliofanya mambo kama hayo atakumbuka hata alisoma chuo gàni?
Mimi Acha niendelee kujiandaa, ñàona Simu ya fundi inaita naamini nguo yàngu itakuwa tayari.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam