Kuna baadhi ya vitu bei huwa kubwa kulingana na usafiri atakao utumia supplier.Mfano mleta mada utaona shipping fee imechangia final price kuwa kubwa.
Either ukimcheki supplier mwambie una Fowarding agent China (Cargo za maji na ndege za kuja Tanzania) Then ongea na hizo cargo mzigo utumwe kwao wao ndio wasafirishe kuja Tz kwa maji au ndege.
Kama unahitaji mzigo mkubwa jaribu kucheki bei 1688 (ingawa iko kichina,ila hivi ni viwanda vya wachina,tofauti na Alibaba ambako wengi ni madalali) ila unasearch unachotaka kwa kutumia picha,Then ongea na watu wa cargo wakununulie then wewe uwalipe Tz.
Hiyo pochi manunuzi pamoja na usafiri ndani ya China kumfikia agent wako pamoja na usafiri kwa njia ya maji toka China kuja Tz inakufikia mkononi kwa jumla ya around 18,000 Tsh.
View attachment 2833421
(Tumia watu wa cargo zaidi,sababu hawa ni watu wenye mitaji,hawawezi kupotea na hela yako.Tofauti na hawa wengi walio instagram wanaokusanya hela za watu na kudai kununulia watu mizigo.Hawa wengi hawako registered Tz,China hawana office,utakuta hata ukimkamata na ukimshitaki hana hata hela ya kukulipa,maana kaila)