HAPANA CHEZEA TZ

Mbolabilika

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2019
Posts
2,128
Reaction score
2,867
Mahakama Afrika Kusini yaamuru ndege ya Tanzania iachwe huru
Posted by: Regina Mkonde 17 mins ago
0 Comments 82 Views
NDEGE ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), aina ya Air Bus A220-300 iliyoshikiliwa nchini Afrika Kusini kwa amri ya mahakama, imeachwa huru. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 4 Septemba 2019 na Dk. Hassan Abbasi, Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia ukurasa wake wa twitter.
Katika andiko lake, Dk. Abbasi amesema ndege hiyo imeachwa baada ya Mahakama Kuu ya Gauteng, Afrika Kusini kutoa hukumu katika kesi ya fidia iliyofunguliwa na mkulima Hermanus Steyn dhidi ya Serikali ya Tanzania.
Dk. Abbasi ameeleza kuwa, katika hukumu hiyo, Mahakama ya Gauteng iliamuru ndege hiyo iachwe, pamoja na mlalamikaji kulipa gharama zilizotumika katika kuiendesha kesi hiyo.
Msemaji Mkuu wa Serikali
@TZMsemajiMkuu
Mahakama Kuu ya Gauteng, Afrika Kusini, leo imetoa hukumu na kuamuru kuwa ndege ya AirTanzania iliyokuwa ikishikiliwa nchini humo iachiwe na mlalamikaji alipe gharama za kesi. Tunawashukuru wote kwa uvumilivu wenu.
Dkt. H.A.
“Mahakama Kuu ya Gauteng, Afrika Kusini leo imetoa hukumu na kuamuru kuwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), iliyokuwa ikishikiliwa nchini humo iachiwe, na mlalamikaji alipe gharama za kesi. Tunawashukuru wote kwa uvumilivu,” ameandika Dk. Abbasi katika ukurasa wake wa Twitter.
Ndege ya ATCL ilishikiliwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo tarehe 23 Agosti mwaka huu, baada ya mahakama hiyo kutoa amri ya kuishikilia kutokana na kesi y a madai ya iliyofunguliwa na Steyn.
 
Utapata tabu sana endeleeni kushangilia na akina mwasiti

Do you understand the words "...interdict #airtanzania airbus from leaving... "?[emoji23][emoji23][emoji23].Mzungu amerudi kotini tenants[emoji23]
 
Do you understand the words "...interdict #airtanzania airbus from leaving... "?[emoji23][emoji23][emoji23].Mzungu amerudi kotini tenants[emoji23]
Furahi tena basi chinja na kuku ufanye na kabash [emoji23][emoji23][emoji23]

 
Mahakama ilisema ndege ishikwe na ikashikwa,
Sasa wamesema ndege iwachiliwe,
ukali wa TZ upo wapi hapo???
Ujui ukali wa TZ upo wapi ngoja nikuoneshe c unajifanya kipofu wewe ,[ Katika andiko lake, Dk. Abbasi amesema ndege hiyo imeachwa baada ya Mahakama Kuu ya Gauteng, Afrika Kusini kutoa hukumu katika kesi ya fidia iliyofunguliwa na mkulima Hermanus Steyn dhidi ya Serikali ya Tanzania.
Dk. Abbasi ameeleza kuwa, katika hukumu hiyo, Mahakama ya Gauteng iliamuru ndege hiyo iachwe, pamoja na mlalamikaji kulipa gharama zilizotumika katika kuiendesha kesi hiyo ]. Kesi kafungua ili apate pesa bado yeye ndo anaetoa pesa na bodo tutamjumlishia na gharama ya muda wa ndege yetu ulivyokaa bila kupiga kazi mbona atajuta kuchokoza Beberu la Afrika mashariki !![emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Its TZ that had lost leverage , and then you went to court, then the same court that ordered your plane to be confiscated ordered it released...ukali upo wapi???? hapa mahakama ya SA ndiyo wanaweza kudai ni wakali, wameshika nchi mzima makende na mkaenda kupiga magoti SA.

Kama TZ ingechukua ndege kutumia njia nyingine kama kuchukua investments za SA zilizo TZ basi mngesema nyinyi ni wakali, au kama Magufuli angeonya SA kutumia mbinu nyingine warudishe ndege...

lakini sasa waliyochukua ndege wamerudisha kwa hiari yao..

This has just exposed the weakness of TZ.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…