Naibu Waziri Mambo ya Nje ya Tanzania, Dk Damas Ndumbaro amesema, Serikali ya Tanzania imeshinda kesi hiyo bila kutoa fedha yoyote ambayo aliyetushitaki alitaka Serikali ya Tanzania tuweke fedha dola milioni 33, kama dhamana.
Kwa upande wake, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dk Hassan Abbas ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba, βMahakama Kuu ya Gauteng, Afrika Kusini, leo imetoa hukumu na kuamuru kuwa ndege ya AirTanzania iliyokuwa ikishikiliwa nchini humo iachiwe na mlalamikaji alipe gharama za kesi. Tunawashukuru wote kwa uvumilivu wenu.
Taarifa za awali zinasema kwamba ndege hiyo hivi sasa ipo njiani kurejea Dar es Salaam.