Hapendwi mtu, maslahi ya Taifa mbele ......... Mswada wa Umeme wakataliwa tena!


Ama imi simjui lakini niliwahi kusoma katika gazeti kuwa baada ya kuteuliwa alisema hajaaza kazi hadi apate maelezo kutoka Ikulu - sasa utajua ni mtu wa aina gani?
 

Nani anayelitia hasara Taifa hili kwa kiwango kikubwa kama sio hao wasomi kwa kukubali kutumikia mfumo ulooza. Msomi wa kiwango cha PhD nafasi yake ni Academician au Researcher ukiona ana nafasi katika afisi ya serikali au siasa ni lazima uweke alama ya kuuliza.
 
Hivi kuna ubaya gani kuruhusu makampuni mengine binafsi ambayo hayana uhusiano wowote na serikali zaidi ya kodi kufanya biashara ya umeme? hiyo bill nafikiri inataka kuondoa monopoly ya TANESCO na kuweka new policy & regulations ya kufanya biashara ya umeme Tanzania,kuna ubaya gani kuruhusu private companies kusambaza na kuzalisha umeme? biashara ya umeme ni kama biashara nyingine tuu kama makampuni ya simu na viwanda,kweli sielewi kwanini bado tunataka kuilinda TANESCO huku watu hawana umeme,ruhusu watu wafanye kazi ndio maana ya nchi huru na sijui faida gani tunapata kwa hizi sheria za sasa za umeme ambazo zimeweza kuweka umeme less than 10% ya population nzima,na kuruhusu kampuni binafsi tusingekuwa na huu ujinga wa Richmond & IPTL,to me hii kitu ni rahisi sana na ningeruhusu siku nyingi sana kuwaachia washindane wenyewe kwa wenyewe kuzalisha na kusambaza umeme kama makampuni ya simu ambayo sasa yanashindana yenyewe kwa yenyewe na serikali ikikusanya kodi kibao...hiyo Tanesco ni kampuni tuu na wala sio kwamba ni big deal sana ikishindwa kazi wengine watafanya kazi,seems wabunge wanachoangalia ni kuilinda Tanesco tuu badala ya kuangalia the big picture,hii kitu inanisikitisha sana maana sioni kwanini bado tuantaka kukumbatia monopoly ambazo hazitusaidii kitu.
 



Unajua we can do better watanzania na watanzania wakapunguza matatizo yao .Nilsha wahi kusema matumizi ya solar Tanzania yanafaa lakini Serikaloi hakitaki kuruhusu uingizwaji wa vifaa ili watanzania wapate unafuu kisa wanataka watu waende Tanesco wakapate pesa.Idrisa shauri serikali ipunguze kodi kwenye vifaa vya solar wengine tupate huduma nje ya tanesco ndiyo tutakuona wa maana.Mnaweka kubwa kubwa na kuwakatisha tamaa watu wa solar why ? Umeme wenu wa shida tuachieni walala hoi tutumie solar .
 
Tatizo sio Ngeleja, Tatizo ni mfumo wa serikali nzima ya CCM, Yeye anatetea yale ambayo Serikali na IMF wanayoyata, hii itakuwa ni sera ya mataifa ya nje tu

Hata kama ni sera ya mataifa ya nje, ina maana tutakubali kila kitu? Mbona kwenye ununuzi wa radar na ndege ya rais mataifa ya nje yalipiga sana makelele lakini serikali ilisimama kidete (Mramba alisema watanzania wako tayari kula nyasi, Mkapa akasema hatuwezi kuendeshwa na mataifa ya nje, JK akasema watanzania wana mahitaji yao wenyewe na wanajua vipau mbele vyao), leo hii hao waliokuwa mstari wa mbele kutetea huo uozo wako wapi kupinga hizo sera ya mataifa ya nje? Au huwa wanapinga sera za nje wanapoona kuna maslahi yao?

Kuna hisia kwamba kuna kitu ambacho kinawekewa mazingira ya utekelezaji (ulaji ama kuingiza mampuni yao). Dr. Slaa anasema walitoa comments za kutosha kwenye huo mswada, lakini bado umerudi mswada ule ule wa zamani, na tena ukiwa na sahihi ya Karamaji. Kwanini serikali haitaki ku-incorporate hizo comments? Mambo yakija kwenda kombo watakuja kusema kwamba sheria ndiyo ina matatizo na kumbe serikali iliweka loopholes kwa makusudi kabisa ili wakitaka kutumia hizo loopholes waweze kufanya hivyo bila matatizo. Hizo sababu za sheria butu ndizo ambazo zinaendelea kutumika mpaka leo kujitetea kwenye sekta ya madini, ukiwauliza kwanini hawataki kufanyia marekebisho hizo sheria mpaka leo hii? Huwezi kupata jibu sana sana utashangaa mikataba zaidi inasainiwa kwa kutumia sheria zile zile ambazo serikali inasema zina mapungufu.

Kwa kifupi ni kwamba pamoja na pressure ya mataifa ya nje, tatizo liko kwenye serikali yetu ambayo inaangalia maslahi binafsi zaidi kuliko maslahi ya Taifa/wananchi. Kama serikali ingekuwa makini na hayo mambo sidhani kama tungejikuta tuko hapa. Kwani TANESCO walipoingia mikataba mabomu kama ya IPTL, SONGAS, AGGREKO, ALSTOM, na RICHMOND kulikuwa na pressure ya maitafa ya nje? Mataifa ya nje yanaweka pressure baada ya kuona kuna mismanagement ya uchumi na kwamba ni nchi masikini ambayo inahitaji misaada ili ku-survive. Tunaweza kuwalaumu hao wa nje kwa makosa ya serikali yetu kukosa umakini kwenye sera na sheria zake ama kuingia mikataba bomu ambayo tumeishuhudia? Kwani hizo sheria, sera na mikataba huwa inatungwa na IMF/WB na donors? Tatizo ni serikali yetu ambayo inaposhauriwa huwa haikubaliani na ushauri huo kwa kuwa ni ushauri ambao unaziba mianya ya ufisadi wakati wao (serikali) wanaona ndiyo opportunity ya KULA!

Safari ni ndefu lakini tutafika tu.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…