Hapo vipi?

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2006
Posts
3,019
Reaction score
579
Nimetafakari niiweke wapi hii story niliyotumiwa na rafiki yangu nikaona labda hapa sawa:

‎Haya tena wandugu katika peruz peruz zangu nimekutana na sababu
nzuuuri za kukufanya wewe na mimi "TUTAFAKARI TUCHUKUE HATUA SAHIHI NA
TUKAPIGE KURA"

1.Rais wa kwanza duniani kudanganywa vibaya mno na wasaidizi wake
2.Rais wa kwanza kuwa na rekodi ya kuanguka anguka mbele ya kadamnasi
3.Rais wa kwanza duniani kufanya safari nyingi za nje ya nchi ndani ya
mwaka mmoja tangu aingie madarakai...ni
4.Rais wa kwanza duniani kutamka hadharani kwamba hajui umaskini wa
watu wake unatokana na nini.
5. Rais wa kwanza duniani kuchakachuliwa mafuta kwenye gari yake
ikazima barabarani
6. Rais wa kwanza anaechukulia wingi wa magari kama kipimo cha maisha bora!
7. Rais wa kwanza duniani anaepata ulinzi wa nguvu za Giza.(mnajimu)
8. Rais wa kwanza aliyesema watoto wadogo wa shule kupata mimba ni
kiherehere chao....
9. Rais wa kwanza anayeogopa mafisadi.
10.Rais wa kwanza duniani aliyetumia mabango yote ya biashara nchini
kwake kujinadi wakati wa kampeni mpaka picha za kampeni

“Every Bathroom has a different STORY.”


 

Haya tena hayo yanaandikwa na mtu mzima, watoto wataandika nini na Taifa hili litakuwa la watu wenye fikra za namna gani!!?. Na unategemea uwashawishi watu wakuelewe katika masuala ya msingi!!!!! I HAVE SOME DOUBTS about the kind of people existing, commenting, voting online and doing other stuff in CYBERSPACE!!
 

Very possible usemayo Truth! Lakini binadamu anazo njia nyingi za kupeleka ujumbe kwa wasikilizaji au watazamaji wake. Ukiangalia kwa makini, japo hakutamkwa mtu kwa jina, yanaelekea kutoa ujumbe fulani. Tutake tusitake ukweli ndio huo. Juzi kwenye TBC1 wanaCCM wawili walipingana wenyewe live. mmoja akisema mwenyekiti wake anatoa ahadi lukuki kila anapokanyaga ardhi na akawa na mashaka kwamba ahadi zote hizo ataweza kuzitimiza katika miaka mitano. Mwenzie kwa kushiba brainwashings za chama za kuamini kwamba chama chao na viongozi wao hawakosei, akasimama alipopata nafasi na kusema kwamba mwenzie aliyetangulia sio mwanaCCM wa kweli, maana asingeweza kutafakari kwa namna alivyotafakari. Hata hivyo ujumbe ulieleweka dunia nzima.

Nadhani mwanaCCM wa kwanza alikuwa sahihi zaidi na ni muungwana zaidi, aliyefuata ndio wale mfano wa vuvuzela, no real constructive message inside, kila anayelisikia vuvuzela anatafsiriyake inayomfaa yeye.
 

Hapo jamaa kweli alichemsha vibaya...

 

MKuu ndio maana imewekwa kwenye jokes, jamani tusiwe serious wakati wote ni muhimu kwa afya zetu.
 
MKuu ndio maana imewekwa kwenye jokes, jamani tusiwe serious wakati wote ni muhimu kwa afya zetu.

Exactly! Huwezi kuzuia nyimbo za taarab kwa kuwa tafsiri ya wimbo mmojawapo unaonekana kukuchoma kumoyo. Jokes ni nzuri kama hazimdhuru mtu na zikachukuliwa kiutani. Lakini mwenye busara haishii kwenye tune ya wimbo bali hutafakari maneno yake aone kama kuna kitu anaweza kujifunza ndani yake. Asipokiona anaupuuza wimbo huo, ila akinung'unika sana watu wataanza kumchunguza zaidi waone kulikoni kaguswa sana yeye peke yake ilhali hakutajwa jina. Ndio raha za starehe zikiwamo jokes. Usiumize kichwa hadharani na jokes kama haikusaidii kukua kifikra. Ama sivyo utamwona kila mtu ni adui wako kumbe sivyo.
 
Hata hivyo sioni kosa kwa huyu aliendika kwamba ni mtoto au mtu mzima, kwani duniani kuna maraisi wengi, hebu mwenzetu tuambie kulikoni kuwa na mashaka na wanajamii. Au umepata ujumbe unaokuhusu ktk hio jokes. Basi ufanyie kazi ndugu afu mambo yaende sawa.
 
Kuna watu wengine hawajui maana halisi ya jokes, wanakurupuka tu na kuanza kulaumu. Mimi namsapoti mshikaji kwa asilimia 9999% Big up
 
Na inakuaje yule rais "mtarajiwa" anaye iba wake za watu (body snatcher)

Na Inakuaje yule mgombea mwenza aliyekimbia umande akaishia darasa la 7 a.k.a LY.

Na inakuaje yule "mbunge" wetu machachari aliye Chifupalize?

Na inakuwaje yule mwenyekiti wetu ambaye ni DJ ambaye kafeli chuo UK hata baada ya kuwa anaandikiwa mitihani?

Lesson: Tukianza kuchambua maisha binafsi ya viongozi wetu mbona tunakesha!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…