pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Siamini kwamba mwaka mmoja umepita, bila ya hasira, visasi, mivutano, malumbano, majibizano na 'makasiriko', kati ya nchi mbili hizi za Kenya na Tanzania. Sio baada ya yote tuliyoyashuhudia, kwa karibia miaka sita.
Yaani tangia mwezi wa nne hivi mwaka uliopita mambo yaligeuka ghafla, yakawa shwari zaidi ya kale kaupepo ka ufukweni. Sasa hivi hata mgogoro wa mwisho, wa Machi mwaka jana, kuhusu mahindi na sumu kuvu tumeusahau kabisaaa.
Hata kile kitendo cha kustaajabisha. Kilichotutonesha vidonda na kupelekea vifaranga visivyo na hatia, vionje ghadhabu kali ya binadamu, tumekizika kwenye kaburi la sahau.
Sijui kitakachofata au hapo mbeleni hali itakuwaje. Ila 'stage' kama hii ndio ile ambayo huwa unawapata wapendanao wakitazama mara kwa mara na kupeana tabasamu za bure. Vicheko navyo huwa vimeshamiri, tena vya kushirikisha meno yote 32, bila ubaguzi. Alafu utasikia, 'baby unajua leo ndio mwaka mmoja umefika tangu tupatane na tupendane?'
Happy Anniversary guys! 🇰🇪🇹🇿🇰🇪🇹🇿