Happy Birthday Bill gates

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,058
Moja ya wajasiriamali waliofanikiwa zaidi Duniani ametimiza miaka 59 siku ya leo.

Katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kuna mambo mengi ya kujifunza labda kwa machache.

1. Mafanikio yanaanza leo...Bill alianza harakati zake za kuwa mmbunifu akiwa na miaka 19 tu, tofauti na vijana wengi wa kitanzania na sehemu zingine ambao wengi wanaamini kuwa na mafanikio ni mpaka ufikie umri wa makamo.

2. Ipo tofauti ya Elimu ya Shule/chuo na ya Maisha.
Bill alidrop chuo na kwenda kulifanyia kazi wazo lake la kutengeneza OPs na lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana tofauti na wazazi au watu waliotarajia kuwa halitafanikiwa labda kutokana na umri wake mdogo na kuacha kwake kumalizia masomo.

Hapa tunajifunza kuwa kumbe unaweza ukasoma na kupata kila aina ya vyeti lakini mwisho wa siku utaaajiriwa na yule mwenye elimu ya kawaida kama Bill alivyowaajiri wanafunzi wenzake japokuwa hakumaliza masomo.

3. Hard work pays.

Kuna watu wanahisi Bill alipata utajiri katika bakuli la dhahabu hadi kufikia utajiri wake Bill alikuwa anafanya kazi sana kiasi cha kufikia kupata muda mdogo sana wa kupumzika chini ya masaa matano kwa siku.

Kuna siku Dada yake Bill alimkuta Bill amelala kwenye meza asubuhi katika ofisi yake, hakuweza kumtambua mara moja alihisi itakuwa moja ya wafanyakazi lakini kumbe alikuwa Bill alikuwa amechoka sana na kulala pale kutokana na kazi ngumu alizokuwa akizifanya.

Hii yote ni ishara kuwa Bill alikuwa anafanya kazi sana kwa moyo lakini mwisho wa siku kazi alizokuwa akifanya zimemlipa na matunda yake yamemfanya kuwa mtu Tajiri zaidi Duniani.

Kuna mengi ya kujifunza kwa Bill, mengine wadau mtaongezea.

Happy Birthday Bill
 
Habarini wapendwa

Leo ni siku ya furaha tunapokumbuka ile siku kuzaliwa
ya Mwanzilishi wa Microsoft ambaye
mtu muhimu sana katika ulimwengu huu wa mitandao
bila yeye tungeyajua haya yote.
La hasha hivyo ungana nami kumtakia heri na afya njema
ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake





Happy birthday Bestito
BILL GATE
 
Sasa huyu ni Bill Gate ni wa humu JF au mwenyewe mwenyewe ?Mungu ampe maisha marefu na amtimilizie haja ya moyo wake
 
huyu jamaa namdai na simu zote kazima,nimeshajiuliza sijui nitampateje
 
Happy birthday bill,you are precious to all Tanzanians .We wish you a very long prosperous life
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…