Nashukuru sana kwa wote walionitakia heri. Naomba radhi kwa kutochangia jana kwani pamoja na kuwa katika siku muhimu kwangu, ilikuwa pia ni siku ya shughuli nyingi za utendaji ambazo zilinichukua hadi usiku wa manane, lakini nilijumuika nanyi kiroho huku nikiiona siku yangu ya kuzaliwa mwaka huu imeangukia katika siku muhimu kwa Waafrika na dunia nzima kwa ujumla kwa kumpata Rais wa Kwanza Barack Obama. Nilijihisi kama Birthday party yangu ilikuwa pale DC.
Nawashukuruni nyote kwa kuwa pamoja katika kipindi chote nilipojitokeza rasmi kuchangia JF pamoja na kuwa msomaji mkubwa hapo kabla. Nawaomba radhi nyote ambao niliwakwaza na kuwaudhi, yote ni katika kujenga, naamini sote tutaendelea kuwa na moyo huo huo.
Sikuwa nimejua kwamba nilijiunga siku chache kabla ya Birthday yangu ya 2007, nashukuru Invisible kwa kunikumbusha. Karibuni sana tuendelee kuwa pamoja.
Shy nakushukuru pia nawe kwa maneno yako ya kuchangamsha, nakumbuka pia ulichangamka zaidi siku ya harusi ya mwenzetu pale Landmark ulipokuwa bize kutaka kutujua tuliohudhuria ukiwa umekaa nyuma ya ukumb. Nilifurahi kukufahamu na nilikusalimu na mke wangu alikusalimu pia japo kwa mbali.