Happy Birthday Lowassa

Habari,

Ni takribani miaka imepita toka Aliekua Waziri Mkuu wa Tanzania kujiuzulu kutokana na kashfa mbalimbali. Nikisoma habari mbalimbali na kuchanganya na mawazo yangu, naamini kuna jambo linaendelea kuhusu kujiuzulu kwa Lowassa na kitendo chake cha kutotaka kuongeleatena kuhusu kujiuzulu kwake.

Kuna kipindi tulikua na City Water ambao walikua ni matapeli. Lowassa aliweza kuwatimua bila kuingiliwa na mtu yeyote. Je kuwatimua kwake ilikua ni kimaslahi sababu hakupewa 10% au City Water walikua na utendaji mbovu, au kulikua hamna mkubwa yeyote aliekuqa na mkono katika ile kampuni?

Nikikumbuka maneno alioyasema Dr. Mwakyembe Bungeni, nanukuu ''kamatungemwaga ukweli wote kuhusu RICHMOND then Nchi isingetawalika''. Kwakauli hii inaonesha kua kuna wengine waliachwa katika list ya RICHMOND ambaowalistahli kuondolewa. Je hao watu ni kina nani?

Katika hiyo list inaoneshahata mtu aliekua juu ya Lowassa alihusika. Hii ni kutokana na imani yangu kua watawalawa nchi ni Waziri mkuu+ walio juu yake.

Pia nikikumbuka maneno aliyoyatoa Lowassa katika kikao cha NEC mwaka jana, nanukuu "Hakuna ambalo lililofanyika kuhusu RICHMOND, mkubwa halikua halijui". Ni ishara kuamkubwa alikua anajua yote yaliokua yanaendela. Sina haja ya kusema mkubwa ninani ila naamini sote tunamjua

Sitaki kusema au kuamini kua Lowassa yuko clean zaidi, la hasha mana hamna alieclean hapa duniani. Naamini kilichomuondoa uPrime Minister ilikua ni njia yakeya kuficha maovu ya wenzake au waswahili wanasema unajitoa Kafara ili uokoewenzako.

Kamayeye hahusiki, ina maana utendaji wake pia ni wa kulegalega kutokana na uwezowake wa kuweza kuwatoa City Water ila kwa RICHMOND alishindwa. Hii ni kutokanana uoga wake wa kuingilia madili ya watu wa kawaida na kuogopa madili ya watuwakubwa. Labda niassume kua hakua na taarifa kuhusu RICHMOND,nayo ni aibu manaviongozi wa nchi mnastahili kuja all about nchii yenu.

Nadhanimkubwa ukitaka waTanzania tujue kuhusu usafi wako na kwamba mambo yote unasingiziwa.Naamini tunahitaji ukweli kuhusu sakata la RICHMOND ili waTanzania tuanzekujenga imani na wewe na si kuweka jambo moyoni na kuamini kua yatapita, manakupita yatapita ila jina lako kamwe haliwezi kusafishika tena.

Kwaufatiliaji wa jambo na utendaji, napenda kukuunga mkono mana You are number 1on that na ndio mana hata Jengo lilipoporomoka kule Chang'ombe, ulimweka ndaniEngineer bila kutaka tuunde tume au tufanye uchunguzi wa kupotza muda na kucheza hela za wananchi.

Hata katikauongozi wako, Shule za Kata zimejengwa nyingi na pia ulisimamia mpaka Chuo kamaMkwawa kimemalizika katika ujenzi na kuanza kutoa elimu. Najua kuna watumtasema vibaya kuhusu Shule za Kata ila naamini imetufanya tusonge kielimu manani heri mtu apate hata hicho kidogo kuliko kukosa kabisa.

Sipo Chama chochote ila nimeyaongelea mazuri na mabaya ya Lowassa na naamini doa lakujiuzulu, akitoa ukweli wote nadhani atatufanya tuanze kujua mbivu na mbichina usitoe pindi ukiona umekosa nafasi ya Kugombea Uraisi mana wananchihatutakuelewa.

HappyBirthday Edward Lowassa
 
Huwezi kusafisha shati jeupe lililochafuka kwa oil chafu kwa kutumia grisi.
 
Mwaka huu mtapambana sana ili kuonekana wazuri, mtapakana sana matope ili kuonekana wabaya...!!!
 
Siasa za ujamaa zilikuwa na nia njema, lakini zilipofika kwa watanzania wakazitumia vibaya matokeo yake ndo haya. Watu wanashangilia mwenge hata faida yake hawaijui. Siasa zimefanywa kama Simba na Yanga, watu wanaleta tu ushabiki bila kujua athari zake kwa taifa hili. Aibu sana.
 
Heri ya kuzaliwa mh laigwanan Lowassa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…