Na Boniface Jacob
Heri ya Kuzaliwa Kamanda wa Anga *FREEMAN AIKAEL MBOWE*......
Kwenye Chama ni Mwenyekiti wetu.
Nje ya Chama ni Mzazi na Mlezi wetu.
Kwenye siasa Ni alama ya Mageuzi Tanzania.
Kiuchumi ni Mtu aliyetoa kila kitu chake kwa ajili ya Taifa lake,Umekuta kwenu Kuna magari,Majumba. Ya kifahari na Chama Tawala walimuheshimu Baba yako Mzee Mbowe......mpaka leo najiuliza hukulizika na nini? Ukajiingiza Kwenye vita hii ya kisiasa iliyochukua kila Kitu chako? Umepoteza Mali,Marafiki,Ndugu,na Amani umebakia nafuraha Kujiamini tuh.
Nakushangaa hata Malipo yako Mengi ni Kejeli,dharau,kushambiliwa na Matusi kwa Unaowapigania ila Ujali!!!!!! Sasa we Mtu gani?
Ningali kijana Mdogo tuh pale UDSM kukaa karibu yako lilikuwa kosa kubwa,Nikajikuta siogopi Mtu yeyote,Wala siogopi tena watawala na Mahakama zao,Jela zao wala Bunduki zao,Nikaanza Kiongea kwa kibesi kama Wewe,Ghafla na Mimi Nahutubia Mageuzi,Hata Mama yangu anajua Ujasiri na Kujiamini kupita kiasi havimo Kwenye Ukoo Wetu,Bali ni zao la Kazi yako.
MUNGU anijalie nione Mwisho wa Kazi uliyoipokea kutoka Mikononi Mwa wazee wetu,Mtei na Bob Makani....Mali zako zimepotea ila Jinalako litadumu Enzi na Enzi.Amin