Happy birthday Ramos

Happy birthday Ramos

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Wakati mashabiki wa Atletico Madrid wanapiga simu majumbani kwao kwa furaha kwamba wameishuhudia timu yao pendwa ikitwaa Ubingwa wa kwanza Ulaya,

Wakati huo mashabiki wa Real Madrid wanamwaga machozi kwamba wamelikosa tena na hili,

Wakati huo muhuni Diego Simeone 'El Chollo' ameyageukia majukwaa ya Estadio Da Luz anainyanyua Lisbon kwamba “amkeni, amkeni, tumewafunga hawa.”

Wakati huo filimbi ipo mdomoni kwa referee 'Bjorn Kuipers', anasubiri fundi mchora ramani kutoka Croatia Luca Modric apige corner yake ya mwisho,

Wakati huo Carlo Ancelotti amemaliza vidonge vyake vya kutuliza Presha, anajua kazi imeisha, nimeshindwa kuwapa Real Madrid taji la 10 la Ulaya.

Wakati huo mtoto Marco Asensio kule jukwaani anamwaga machozi, kwamba tumefungwa na watani zetu.

Alikuwepo mwanaume mmoja na mawazo tofauti. Maisha yake ni Madrid, mwili wake ni Madrid, hakuwa tayari kushuhudia wakifungwa tena akiwa nahodha.

Kichwa chake kiliupeleka mchezo dakika 30 za nyongeza na Madrid waliondoka na UEFA yao ya kumi.

Sergio Ramos is 35 today.
HAPPY BIRTHDAY
deo_mwanasoka-___CNDP4vCKyEX___-.jpg
 
Back
Top Bottom