Page 94
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 5,204
- 15,207
If others has to die to let others survive; I believe mama had died to let me live.
Ikiwa Leo ni siku ya kumbukumbu yangu ya Kuzaliwa, pia ni siku ya kukumbuka mapumziko ya milele ya Mama yangu.
Mara nyingi, imekua ni siku ya furaha kwa Kuzaliwa, lakini majonzi na simanzi ziliizidi siku ambayo nilizaliwa. Mama na tegemeo La wengi, aliondoka angali akihitajika mno. The moment I was out, was the moment she has rested in an eternal peace.
Imekuwa ni ngumu sana kufanya hii ni siku ya kumbukumbu ya Kuzaliwa, badala yake imekuwa ni siku ya kukumbuka kifo cha mama.
Pamoja na yote, imekuwa ni siku muhimu sana. Siku ambayo hutuweka pamoja na kutuunganisha sote kama familia. Siku ambayo, kila mmoja huacha majukumu yake na kujumuika pamoja katika mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na sala na mengineyo.
Katika siku hii muhimu, utukufu umfikie Mwenyenzi Mungu,shukrani nyingi ziwafikie wote ambao wamenifanya kuwa hivi nilivyo Leo.
Zaidi, shukrani za kipekee zimfikie Mama- Dada yangu 'Neema',
Kwa jitihada zake za kipekee za kunikuza bila ya kuhisi kupungukiwa na chochote. Upendo wake usio na kikomo ndiyo nguzo ya ukuaji wangu mpaka umri huu.
Dada yangu ni Mama Yangu
Mungu awabariki wote na Mwenyenzi Mungu ampumzishe mahali Lema peponi mama yangu kipenzi.
Happy Birthday to me. Rest in peace Mama.