View attachment 1000296
Picha ya Kampeni 2020
Siku kama ya leo miaka 51 iliyopita (mwaka 1968) Mungu aliipa Tanzania zawadi. Zawadi hiyo ni mtoto ambaye wazazi wake walimuita Tundu. Amededicate maisha yake yote kusaidia watu. Aliletwa kwa kusudi maalumu, na anaishi kutimiza kusudi hilo. Si Rais wa nchi, Rais wa TFF wala Rais wa Manzese watakaoweza kuzima kusudi hilo.
Mwaka juzi (2017) hayawani wachache, wenye roho za kinyama wakiongozwa na hayawani mkuu walijaribu kuzima kusudi hili la Mungu. Risasi 17 za SMG mwilini, huku nyingine 19 zikimkosa lakini hawakuweza kutimiza mpango wao huo wa kishetani. Mungu akasimama na kuonesha ukuu wake.
Nilipomtembelea Nairobi nilimwambia 'wewe ni muujiza unaoishi (a living miracle). Mungu alikuleta duniani kwa kusudi maalumu na hutaondoka hadi utimize kusudi hilo. Najua wapo wanaonuna kusikia hivi, na tumeanza kuwaona wakiandika 'viwaraka uchwara' vya kinafiki kujifanya eti wamekumiss baada ya kupona. Mungu atawajibu kwa moto.
Heri ya siku yako ya kuzaliwa my brother. Mungu akujalie maisha marefu utimize kusudi lake. Happy birthday the living miracle Tundu Lissu
Credit Malisa GJ