Happy Left Handers Day:13/08

Vegetarian

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2012
Posts
654
Reaction score
509
Leo 13/08 /2016 ni siku ya kimataifa ya watu wanaotumia mikono ya kushoto na hata miguu pia. Naomba niwatakie heri ya siku hii wana JF wote wanatumia mikono/miguu ya kushoto .
Duniani kote inakadiriwa kuwa 10% pekee ndiyo wanaotumia mikono ya kushoto. Sababu ya uchache wao, wamekuwa wakisahaulika kwa sababu vifaa vingi vimebuniwa kwa ajili ya watumiaji wa mikono ya kulia. Hali hii wakati mwingine imehatarisha maisha yao. Kwa upande mwingine, pamoja na uchache wao wapo watumiaji wa mikono ya kushoto waliofanikiwa kufanya mambo makubwa duniani. Baadhi yao ni:
-Barrack Obama
-Bill Clinton
-Bill Gates
-Steve Jobs
-Oprah Winfrey

-Benjamin Netanyahu
Wengine katika historia ni Leonardo da Vinci, Isaac Newton, Thomas Edison, Albert Einstein, Charles Darwin..
Pia kuna wengine kama Osama Bin Laden, Jack the Ripper pia walikuwa wanaotumia mikono ya kushoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…