Mother love is the fuel that enables a normal human being to do the impossible. ~Marion C. Garretty, quoted in A Little Spoonful of Chicken Soup for the Mother's Soul
THERE IS APOWER IN MOTHERS TO PROTECT LIFE!!
Nakumbuka siku moja nikiwa Morogoro (nimechoka na mwili unahoma) nasubiri basi,nikitokea Dodoma nikielekea Mbeya, nilimwona mama mmoja pale stendi ya Msamvu yuko na rambo yake ameshindilia nguo na vingine humo pamoja na mtoto wake mkononi akiwa analia. yule mama alikuwa akihangaika sana kumnyamazisha. Punde nikamwona anakwenda okota ndizi iliyotupwa na abiria aliyekuwa ndani ya basi linaloondoka la Abood. aliirudi upesi kwenye rambo yake akatoa kijiko na kuanza kuiparua ile ndizi kwa nje kisha akampa mwanae. yule mtoto (umri wake ni chini ya mwaka) aliifukamia kwa nguvu sana. Jambo lile lilinishitua mno, Nikakumbuka, nalikuwa mtoto kwa mama. nikajiuliza hivi mama yangu nikiwa na umri kama huo alipitia maisha yanayofanana na hayo? ghafla, machozi yalianza kunitoka. Kwakuwa nilikuwa nimekaa chini tena nimejikunyata, nilipokuwa nafuta machozi hakuna aliyejua. nikiisha jifuta hayo machozi nilikwenda kwa huyo mama kumuliza kulikoni. akanijulisha kuwa kafukuzwa na mumewe walikuwa wanaishi "Kihonda" siku ya nne sasa analala nje ya nyumba. Sasa ameonelea bora arudi nyumbani Iringa lakini hana pesa yoyote. Tuliingia kwenye vihoteli vya pale pembeni nikamnunulia chakula chake na mwanae. Yule mama hakutaka vyakula vije sambamba, aliomba kije cha mwanae kwanza akamlisha. Kilipokuja chake mtoto akadandia kidogo tu kisha akakataa. Ndipo mama akala. Muda si mrefu mtoto akalala.