Happyness Magesse anaulizwa Kiswahili anajibu Kiingereza


limbukeni tu wewe
 
mhh mkuu sidhani kwamba kuchanganya english na swahili ni big deal!!! system ya elimu yetu ndio yakulaumu primary kiswahili, secondary school english, univerities english, business- swahili, maofisini etc
Naamini yule dada angeongea Kiswahili labda hapa na pale akachomeka neno la Kiingereza kama tulivyo wabongo sidhani kama watu wangelalamika kwani lugha ambayo angekuwa anatumia ni kiswahili. Shida ya yule dada na ambayo imekera watu ni kuamua kuzungumza au kujibu kwa Kiingereza badala ya Kiswahili, na mahali alipokwama ndo akawa anachomeka maneno ya Kiswahili. Kumbe lugha kuu ya mazungumzo yake ilikuwa Umombo. Hili ndiyo tatizo.

Watu wanajiuliza, je, ilikuwa busara kuulizwa kwa Kiswahili yeye anajibu Kiingereza wakati hadhira yake ni watanzania ambao lugha yao ya taifa ni kiswahili?
 
mimi nakubaliana na wanaosema hapa kwetu bongo kuzumngumza kiingereza ndo unaonekana msomi na ukitaka kupata kazi kwa wepesi we uwe unajua lugha hiyo hata kama kichwani ni mtupu huyo megese alichokuwa anakifanya ni kuwakoga wabongo ajiangalaie kuna watu wanaifahamu hiyo ngeli kama wamezaliwa UK kuna watu wako state huko Uk zaidi ya miaka kumi sasa na bado wakipiga simu bongo wanaongea kiswahil itakuwa yeye wa juzi halafu hapo bondeni kw madiba ambako watu wanzungumza kizuru na kiingereza lazima muungwana ujue hapa mahaojiano yangu ni kwa ajili ya watanzani na sio waingereza na ndio maana mi redio mingi yamavipindi ya kiingereza yamefeli na kuicha 88.4 inapeta mpaka kesho ni vyema ujue hadhira gani unayoikabili kw wakati huo aache ushamba wake msukuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…