Qualifier
JF-Expert Member
- Dec 14, 2012
- 1,252
- 405
Ndugu zangu wana jf hasa walioko sekta ya Elimu ninakumbuka kuna wanaharakati walitaka kuanzisha chama cha walimu kitakacho simamia maslahi ya walimu sawa na ilivyo kuwa CWT ya mwanzo kwani sasa CWT imebeki kuwa historia tu nakuwa chama cha wanyonyaji wanaotumia jasho la walimu kujengea majumba na kununua magari ya kifahari huku wakishindana kutumia magari ya kifahari na kuwaacha walimu wakiwa hawana mtetezi wa maslahi yao. tazama madeni ya walimu limekuwa tatizo sugu na CWT wamekaa raha mstarehe , huku serikeli ikiendelea kuto wapandisha madaraj walimu, na hata wale wanao pandishwa hawalipwi mishahara mipya kwa miaka kadhaa na wanapo dai maqlimbikizo yao wamesimama kila moja peke yake kama vile hakuna chama cha walimu.sasa je wale wanaharakati walioonyesha dhamira ya kuwa komboa walimu kutoka cham hiki ambacho sasa kimekaa kibiashara na kusahau wajibu wake wamezimwa na nini?sisi walimu tuko tayari kabisa kuhama kutoka chama hiki ambacho kimepoteza kabisa dira wa CWT.na ninawashsuri walimu wanao ajiriwa ajira mpya wawe macho na hawa matapeli.maana wataanza kupita na fomu huku kwakitoa maneno matamu ambayo ni kinyume kabisa na hali ya kiutendaji wa CWT ya sasa. haiwezekani madeni ya walimu yakae muda mrefu hivi na baadae hata kama serikali itatulipa ni baada ya muda mrefu sana huku thamani ya fedha ikiwa imeshuka sana. Hebu wanaharakati endeleeni tuko nyuma yetu pengine kuna siku mwalimu wa Tanzania atakuja kupata ukombozi.