Nono6135
Member
- Jun 14, 2024
- 13
- 21
Utangulizi
Kumekuwa na harakati nyingi za kutetea haki za mtoto wa kike ambazo chimbuko lake ni kuwepo kwa mfumo ambao ulimpa kipaumbele mtoto wa kiume (Mfumo dume). Mfumo huu ulijengeka na kuwa sehemu ya utamaduni na maisha ya kila siku. Juhudi nyingi zimekua zikifanyika na zinaendelea kufanyika kuhakikisha mtoto wa kike anakuwa sawa na mtoto wakiume (usawa wa kijinsia). Juhudi hizi zimesaidia kuinuka kwa mtoto wa kike lakini wakati mwingine kwa kumsahau mtoto wa kiume ambapo ni kinyume cha usawa wa kijinsia. Hivyo makala hii itachunguza chimbuko na juhudi za utetezi wa mtoto wa kike na changamoto zake hasa kwa kumulika mapungufu dhidi ya mtoto wa kiume katika kupigania usawa halisia wa kijinsia.
Historia ya utetezi wa mtoto wa kike
Kulingana na hali iliyokuwepo toka enzi na enzi, siyo siri kuwa mtoto wa kike aliachwa nyuma katika nyanja mbali mbali, za kijamii, kiuchumi, kielimu na kisiasa. Hii ilitokana na mila na desturi katika jamii, mifumo ya kisiasa na kiuchumi ambayo haikumjali sana mtoto wa kike. Dunia ililiona hili na kuanzisha harakati za usawa wa kijinsia. Mfano ni karne ya 18 “A Vindication of the Rights of Woman” (1792); Mkutano wa Seneca Falls (1848) - mkutano wa kwanza wa haki za wanawake; International Council of Women (ICW) (1888) - moja ya mashirika ya kwanza ya kimataifa ya wanawake, likitetea usawa wa kijamii, kiuchumi, na kisiasa; Tamko la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji (1995). Nimetaja machache.
Baada ya Jukwaa la Beijing juhudi za utetezi juu ya mtoto wa kike zilishika kazi karibia dunia nzima ikiwemo Tanzania. Tanzania kumekuwa na juhudi za kisera na kisheria, vyama na mashirika ya kutetea mtoto wa kike mfano: Tanzania Media Women’s Association (TAMWA); Women Fund Tanzania (WFT); TGNP Mtandao (Tanzania Gender Networking Programme); Women’s Legal Aid Centre (WLAC); Association of Women Lawyers (TAWLA) Elimu kwa Mtoto wa Kike (CAMFED - Campaign for Female Education, na FAWE - Forum for African Women Educationalists); hivi karibuni Udhamini wa Raisi wa Tanzania kwa watoto wa kike vyuoni maarufu kama Samia Scholarship.
Juhudi hizo zote hapo juu ni sahihi sana lakini dunia inaendelea kushuhudia juhudi hizi bila kikomo na bila kugeuka na kuweka juhudi za kuleta usawa wa kijinsia halisia kiasi kwamba utaibuka mfumo jike ambao itakuwa vigumu kupamabana nao.Ugumu utatokana na ukweli kwamba mfumo huu utakuwa umejengewa miundo mbinu (sera, sheria, miongozo na matamko) tofauti na mfumo dume ambao ni kama wa asili. Dunia inashuhudia nguvu nyingi zikiwekezwa kwa mtoto wa kike kana kwamba mtoto wa kiume anayezaliwa leo bado anakuwa na nguvu ya kuendeleza mfumo wa kumuweka nyuma mtoto wa kike wakati miundo mbinu imebadilika. Hali hii yaweza kusababisha changamoto.
Ni zipi Changamoto Tarajali?
1) Kuibua Vita ya Kijinsia. Kutokana na wanaume kuzidi kusahaulika na nguvu nyingi kuelekezwa kwa wanawake katika sera na mipango ya maendeleo kunaweza kuibuka siasa za kijinsia ambapo kutakua na upinzani mkubwa kutoka kwa wanaume kwa siku za usoni na mapambano yasiyo na tija kwa jamii.
Kupuuza Masuala Yanaoathiri Mtoto wa Kiume. Kutotambua na kushughulikia masuala ya mtoto wa kiume mfano afya ya akili inayoletwa na matarajio ya jamii kwa wanaume hata kama uwezo wa asili hakuna.
2) Mwanaume mara nyingi anatarajiwa kufanikiwa katika kazi zake ili kuthibitisha thamani na uwezo wake. Hali hii inasababisha msongo wa mawazo kwa baadhi ya wanaume na hivyo kusababisha matatizo ya afya ya akili. Nguvu kidogo inaelekezwa katika eneo hili wakati hili ni bomu linaloripuka taratibu.
3) Kuongeza Wanaume Wasio na Ajira. Kutokana na ukosefu wa usawa wa kijinsia kwenye ajira ambapo katika baadhi ya sekta kwenye jamii kumekua na hamasa kubwa na mipango mikakati ya kuajiri wanawake zaidi, hali hii inaweza kusababisha wanaume kusahaulika siku za usoni.
4) Migogoro ya Kijamii. Kuzingatia haki za jinsi ya kike bila kuangalia kiume kunaweza kuibua migogoro ya kijamii unyanyapaa kwa mtoto wa kiume. Ambapo baadhi ya wanaume wanaweza kuhisi wanapuuzwa na hivyo kuleta chuki na mgawanyiko wa kijinsia.
5) Ongezeko la Vijana wa Kiume Wenye Tabia Hatarishi. Tabia kama matumizi ya madawa ya kulevya, wizi, ubakaji, ushoga na ujambazi zaweza kukithiri. Juhudi za kuwanusuru vijana hawa wa kiume bado hazijawa mahususi kama zile zinazoelekezwa kwa mtoto wa kike.
Yapi Mapendekezo ya Usawa wa Kweli?
1) Kuhamasisha usawa wa kweli wa kijinsia. Tupunguze au tuache kabisa utetezi wa mtoto wa kike unaotusaulisha uwepo wa mtoto wa kiume. Tuhubiri usawa wa kweli si upendeleo wa jinsi moja. Hili lifanyike kwa kuelekeza sera, sheria, kanuni, taratibu na matamko kiusawa sawia kwa kumwangalia mtoto wa kike na wa kiume kama mwanadamu mwenye mahitaji sawa isipokuwa ya kibaiolojia hasa ya kiuzazi.
2) Kutoa fursa sawa za ajira kwa wanaume na wanawake. Kwasababu mifumo na mtazamo umebadilika katika jamii kwa sasa hivyo serikali inapaswa ihakikishe kuwa inawezesha jinsia zote kiuchumi na katika upatikanaji wa ajira kwa mtoto wa kiume na wa kike. ili kuepusha vijana wengi wakiume kubaki bila ajira.
3) Serikali kupitia waziri wa vijana na waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na makundi maalumu lazima izingatie umuhimu wa kuwapa kipaumbele jinsia zote hasa katika hiki kipindi cha wimbi la afya ya akili na pia kutoa elimu ya afya ya akili katika jamii ili kupunguza matukio mengi yatokanayo na kusahaulika hasa kwa wanaume kama vile kujinyonga.
4) Serikali pamoja na mashirika ya kijamii wafanye juhudi za kuweka mfumo maalumu wa kufuatilia, kutathmini nakuhakikisha kuwa juhudi za usawa wa kijinsia zinafanikiwa bila kuathiri jinsi yoyote.
5) Usawa wa kijinsia ufanyike kwa matendo. Serikali ihakikishe maisha yote ya Mtanzania yanatawaliwa na usawa kadiri ya uhitaji bila kujali jinsi. Hii itasaidia kubadilisha mtazamo wa kuonesha kuwa wanawake pekee ndio hutetewa.
Hitimisho
Ingawa kunaonekana changamoto za kutilia mkazo usawa wa jinsi moja, bado inawezekana kufikia usawa wa kweli wa kijinsia kwa kuhakikisha kuwa juhudi zote zinazingatia mahitaji ya jinsi zote. Kwa kufanya hivyo, Tanzania itajenga jamii yenye usawa wa kweli na maendeleo kwa wote kwa miaka ijayo bila manung’uniko.

Upvote
114