Pre GE2025 Harakati za RC Juma Homera katika jimbo la Namtumbo, zinaharibu kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Vita
 
Acha kumchafua, kama una msuli compete naye.
 
Kuna mambo mengi yanakwama hapa Mbeya. Wananchi bado wanalalamika na Gharama za Maisha, Sukari haishikiki.

Mtu ambaye angesaidiana na Wakuu wa Wilaya kusimamia haya ni Mkuu wa Mkoa. Ajajbu mkuu wa Mkoa anamaliza hata Wiki mbili yupo Songea na Namtumbo kufanya Ushawishi wa Ubunge ili agombee.

Watu kama hawa wanashindwa kumsaidia rais kila siku Malalamiko. Hakuna anayejali Mwananchi wa Kawaida.

Rais anatakiwa awachunguze wateule wake. Yeye anajua ana mtu Mbeya kumbe ni bure.

Homera achague moja Ubunge au Ukuu wa Mkoa. Sababu anawaumiza Wananchi wa Kawaida. Hizo hela anazogawa huko si atujengee barabara Korofi japo tumkumbuke kwa hilo?

Kila ukienda Ofisini kwake hayupo, Ukiuliza yupo wapi wanasema kaenda Namtumbo Mkoa wa Ruvuma kufanya vikao vya chama.

Kwani Mkoa wa Ruvuma hauna Mkuu wa Mkoa?

Na hii Rais Samia akijua anaweza kupoteza hata huo ukuu wa Mkoa.
 
Tulishasema Wakuu wa Mikoa hawana kazi. Kwenye Katiba Mpya watakuwa redundant.

Na ukweli ndiyo huo, hayupo Mbey na mkoa haujatikisika.
 
Unamsagia kunguni sio. Homera hatolewi hapo, angekuwa mto tofauti wangeshakula kichwa tokea mwaka jana Rais alipokuja hapo. Lakini mama hana baya.

Kuhusu kuondoka ondoka hiyo haina shida maana hata Rais hajakaa nchini siku za kutosha tu na mambo yanaenda. Itakuwa mkoa wa Mbeya.

Muachani akatafute marisho mapya awaachie nafasi wengine hapo.
 
Ukuu wa mkoa ni supana mkononi, any tm unaliwa kichwa.


Mwenye mkoa ni RAS akishirikiana na RSO, RPC, na makatibu tawara wasaidizi.
 
Mnamnanga tena?Siyo huyo aliyemwagiwa sifa kama gunia nne kwa ufanyaji kazi mwema?NB;Sukari na umeme mmefikia wapi huko?
 
Mwandishi inaonekana wewe ni mpambe wa Mbunge wa sasa wa jimbo la Namtumbo maana kwa namna ulivyoandika ni wazi lengo ni kumchafua RC-Juma Homera.
Sukari kwa sasa ni issue ya Kitaifa mpaka Waziri mwenyewe hana majibu ndio itakua RC !
Umeandika kuwa watu wanamtafuta RC ofisini hayupo je hakuna anayekua ameachiwa ofisi na RC ?
Je wanakwenda kumtafuta RC au Juma Homera. Maana RC akisafiri RAS yupo na ndiye mtandaji mkuu wa Serikali ndani ya Mkoa.
Muda huohuo unaandika kuwa RC-Juma Homera anatoa rushwa huko Namtumbo..yaani hapo hapo una shida na RC-Juma Homera kule Mbeya muda huo huo una taarifa za yeye kutoa rushwa na kutengeneza mtandao kuelekea uchaguzi 2025 ?
Mwambie Mbunge wako aendelee kuzichanga karata vizuri badala ya kukutuma kuchafua watu.
Kwa namna ulivyoandika iko wazi sana kuwa wewe upo upande wa Mh: Vita Kawawa na lengo lako ni kumdhoofisha J.Homera.
 

Wapiga kura wa CCM
 
Rais anaona ila huwa hafanyii kazi majungu
 

Mnamwonea Homera, huyu ni kijana poa sana, hana maringo, msikivu na hana makundi.
Inaelekea wewe uliye Ruvuma unamuogopa.
 
Kwani Homera ndo aliyesababisha ukosefu wa sukari nchini?Mwulizeni Raisi kwa nini hakuna sukari.Nyinyi wananchi wa mbeya mna shida sana.Tatizo ni ukabila unawasumbua.sukari iko hapo tunduma,kyera tena nyingi tu si mkanunue huko?Najua TRA wanasumbua sana kuingiza hiyo sukari lakini si kuna njia nyingi tu za panya?Kama nchi haifuati sheria kwa nini wananchi wazifuate!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…