Harambee: Kuiona Mechi ya Brazil na Taifa stars

Zion Daughter

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2009
Posts
8,921
Reaction score
4,240
Kwanza kabisa napenda kuchukua fursa hii kuipongeza serikali kwa juhudi iliyofanya kuhakikisha kuwa Brazil wanakuja bongo kutupa raha ili tusahau machungu ya maisha makali.Lakini kwa upande mwingine nimeshtushwa na viingilio kuwa vikubwa sana kuzidi uwezo wangu na nisingependa kuikosa historia hii.Sasa basi ombi langu ni toa ndugu ili angalau nipate laki na nusu za kutizama mechi hiyo.
Mchumba wangu Krispin hana uwezo wakutosha kwani anabeba mizigo(sio maboksi jamani) na isitoshe yeye priority yake kubwa ni therengeti therengetiiiiii na chui!!!!
Nimeweka kwenye jukwaa hili la mahusiano kwa vile najua mna upendo sana na hamtanipotezea wala kunidiskaregi kwa namna yoyote.
Natumaini nitapata wafadhari wa kunipeleka kuona pambano na ikizingatiwa kuwa sijawahi kuingia Neshno stadium na hii itakuwa bonge la chansi kwangu.
Mwisho kabisa natanguliza shukurani za dhati kwa wapwaz na mabinamuz Geoff,bht,Nguli,Nyamayao,FL1,Balantanda,Fidel,Kaizer,mchumba na wengine woooote.......(i know you will not let me down).
Asanteni.
 

Hujanitaja, ungenitaja ungelamba tiketi ya 150, kitopu cha jezi ya Taifa Stars na bia za kopo za kunywa uwanjani ili kupandisha mzuka wa kushangilia. Kwa kifupi imekula kwako!
 
Charity mie nishaanza kumuomba Fidel80 anilipie anadai nikifika ukumbini nisiombe hata maji ya kunywa .
200,000.00
150,000.00
*
*
*
*
50,000.000
*
*
*
*
30,000.00 :rolleyez:
 
Nimetoka kuchangia, kipaimara, Komunio, Harusi, Mchango wa choo cha shule na nyumba ya mwalimu, nimechangia CCM ishinde, nimechangia wahanga wa Mafuriko, send off, Kitchen party, mchango wa ulinzi kwenye mtaa.....sasa mchango wa kuona Brazil naomba unisamehe kwa hili.....
 


Kutoa ni moyo...
 

Sikutegemea mkuu ungeweza kuchota maji bwawani kwenda kuyajaza baharini...!!
 
Hujasema uko mkoa/nchi gani ili nikuandalie na sehemu ya kufikia hapa jijini!!
 


noted with many thanks mkuu,,,ndo ile ya sms nini? sh300 LOL

charity usijali mi nitakuchangia ukaone mpira shemeji japo sitaenda. Utaenda na hommie wangu Xpin au mwingine?
 
noted with many thanks mkuu,,,ndo ile ya sms nini? sh300 LOL

charity usijali mi nitakuchangia ukaone mpira shemeji japo sitaenda. Utaenda na hommie wangu Xpin au mwingine?

Kaizer mbona hupatikani popote ...........aaaaaaaaaaaagggggh
 



Usiache mchango wangu mara baada ya kufikisha 195,000
 
MASAKI:Nimekutaja angalia vizuri kwenye post yangu,upo kwenye na wengine woote.Najua wewe utanifadhili kofia na traksuti.

FL1:tupo pamoja mama,WANAWAKE na michezo

MASANILO: kutoa ni moyo,haijalishi umetoa kwa wangapi,hata Yesu aliutoa uhai wake kwa ajili yetu.

BROOKLYN : Mie ni WAHAPAHAPA bongo tambarare

Shemej KAIZER : asante kwa pleji yako,umeonesha njia kuwa INAWEZEKANA.

NB.Naomba michango yote ipokelewe na Mwaka hazina bht, au wasiliana na makamu mweka hazina FL1 vilevile mwaka hazina msaidizi JS.
Nawashukuru tena kwa moyo wa ukarimu.
 
1.ina maana mchango ukiishia 30,000 hutaenda?
2.wewe una sh ngapi kianzio?
3.Ulishawahi kwenda mpirani kuona mechi yoyote ya kimataifa?
4. Nia yako ni kuona mpira au pesa ya kuona mpira? kumbuka kuna free pass kibao!!!!!(sijasema ninazo)
 

Haya best nitakuchangia baada ya mechi maana nimebanwa sana sijui hata kama mwezi huu nitaweza wakilisha mchango wangu kwenye ule mchezo wa ofisini kupeana!
 
1.ina maana mchango ukiishia 30,000 hutaenda?
2.wewe una sh ngapi kianzio?
3.Ulishawahi kwenda mpirani kuona mechi yoyote ya kimataifa?
4. Nia yako ni kuona mpira au pesa ya kuona mpira? kumbuka kuna free pass kibao!!!!!(sijasema ninazo)


1.This is my chance ndio maana ningefurahi sana kama angalau ningekaa kwenye jukwaa la laki mbili,huko Kamera ya CNN,SKAI NEWS na BBC inaweza kunipitia(sore ofutopiki).
2.Mie sina chochote ndugu yangu ndio maana nikaona niombe mchango,wahenga walisema mficha nanihii hazai.
3.Sijawahi kuingia uwanja huo wa taifa ndio maana nimeomba msaada huu niweke historia achilia mbali kuona mechi za kimataifa(labda kwenye luninga)
4.Nia yangu ni kuona mpira hivyo nikipata free pass nitashukuru pia.(ila hela ya maji ya kunywa uwanjani nayo ni muhimu)
Nadhani nimejibu vema tall.
 
Pitia uchukue carton ya Konyagi hapa ukauze Bar yoyote najua hukosi si chini ya 100000.
 


Kwa mvao huu wa asili ya Mtanzania nina uhakika Bodi ya Utalii Tanzania itakupa free pass ili Wabrazil wapate fursa ya kuona mavazi yenye asili ya Kitanzania. Sasa watakuonaje kama usipokaa VIP ambako ndipo wanapoingilia na kutoka uwanja? Kwa kifupi umeshapata free pass na utakuwa na JK pale jukwaa kuu !

Kingine?
 
Pitia uchukue carton ya Konyagi hapa ukauze Bar yoyote najua hukosi si chini ya 100000.
Nashukuru sana kwa ukarimu,ila tatizo ni kuwa hizo mila za konyagi kwenye kabila yetu hazipo.Hivyo hiyo biashara itakuwa ngumu.Naomba mchango mwingine tafadhari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…