Harambee: Kuiona Mechi ya Brazil na Taifa stars

ila ukiiangalia kwa undani mada hii utakuta wote wanaongelea kitu kimoja lkn kwa mtazamo tofauti
 
Kiranga.......i wish jk angepitia shule ulizopitia wewe....
Honestly.........

Tatizo sio shule....tatizo ni common sense hakuna vichwani mwa Watanzania wengi. Huyu mwanamke aliyeanzisha hii mada ni microcosm ya jamii nzima kwa ujumla. Mbaya zaidi common sense haifundishwi shuleni wala kununuliwa dukani. Unaweza ukawa na miakili kibao ya kwenye mivitabu lakini akili ya maisha, busara, na hekima huna. Unaweza ukawa na mihela kibao lakini common sense huna.

Kuna ugumu gani kuona kuwa hiyo ada wanayoilipa Brazil ni matumizi mabaya ya fedha chache tulizonazo wakati tuna matatizo makubwa na mengi yanayotukabili? Napenda sana kumtumia binti yangu kama mfano kwa sababu ana common sense nyingi sana na hata yeye angeliona hili. Inakuwaje mijitu mizima na akili zao hailioni hili hadi kuunga mkono kitu cha kipumbavu?
 

Fact ni kwamba you can't get something out of nothing, at the very least utu wa ombaomba unapungua.

Ndiyo maana hata watoto wa nursery wanafundishwa wimbo huu.

"Kuomba omba, kubaya sana, kuomba omba, kubaya sana
Usiombeee, usiombeee, jitegemee"

Zaidi, tunajua kwamba shida haina mwenyewe na kuna nyakati inabidi kuomba, lakini si katika anasa kama hizi.

What I know about Charity ni kwamba kaja hapa kupalilia tabia ya uombaomba, uomba omba usio tija, wa gharama zisizo msingi, gharama za starehe za mpito, anataka kuwatia watu mzigo usio lazima.

Lazima tupinge upuuzi kama huu maana mawazo ya kipuuzi kama haya ndiyo yanayorudisha nyuma taifa letu, badala ya wananchi kufanya kazi wanakuwa wanategemea kuombaomba, kwa jirani, kwa serikali, kwa mjomba.

Naamini katika uhuru wa matumizi ya mtu na pesa zake, lakini Charity hana pesa zake anazotaka kutumia hapa, anataka kuchangisha wenzake, kwa hiyo uhuru wa matumizi hana hapa. Na ni kweli watu wana hiyari ya kumpa au kutompa, lakini mtu akishakuwa ombaomba akubali kuambiwa ukweli kuhusu hiyo tabia yake, hususan kama anaendekeza uomba omba kwenye mambo ya anasa za gharama zisizo lazima. Mimi nafanya kazi ya kusema ukweli tu hapa.

Si maisha hayo, lazima tujirekebishe.

Kesho keshokutwa mtoto atakosa maziwa kwa sababu mama kaweka relaxer kwenye nywele, priorities.
 

Right on point my dude, right on point.

Ndiyo maana nikasema hizi ni first principles tu.

You can't get something out of nothing.

You shouldn't try to live above your means.

Always try to pay your way, and if you can't pay for something, avoid it, work more, use your brain in legit ways, save until you can then get it. That's why people have layaway and shyt, to instill financial discipline and ensure you only get what you can pay for.

Heck, mbona ni vitu fulani basic tu?

Tatizo letu tunataka kujiachia sana. Tunataka tuwe ombaomba halafu hapo hapo tunadai tuheshimiwe, eti tuna dignity.

Dignity iko wapi? Ukishaanza kuombaomba ndiyo ushaitupa dignity tayari, hususan kuomba omba huku kusiko na akili, kichwa wala mguu.

Kama nilivyosema hapo juu na wakuu wamenikubali, kama dada yetu angekuwa ameshikwa yuko lupango, kasingiziwa, hana bail money, mimi namjua dada clean, heck, hata milioni watu wanatoa.

Kama dada anaenda shule, anataka kufukuzwa, hana ada, heck, mbona ubinadamu ninao tu, trackn record inanisemea wala sijisifii.

Lakini haya ya kwenda kucheza mayenu na kuona Samba?

Kwani akikosa atapa kilema?
 
ila ukiiangalia kwa undani mada hii utakuta wote wanaongelea kitu kimoja lkn kwa mtazamo tofauti

Unaweza kufafanua? Yaani mimi ninayepinga ombaomba anayeendekeza anasa na hao wanaomtetea tunaongea kitu kimoja?

Unaweza kunielimisha kivipi?
 



Charity hajamtia mtu mzigo usio lazima kwani hajamlazimisha mtu, ...nimekwambia pale juu kuna watu wanazo pesa in excess...kama kwako hii ticket ni 'mzigo.gharama usio wa lazima' kuna wengine...hii ni hela mbuzi tu,na sio mzigo!

Humjui charity,hukupaswa kumdhalilisha,kama kuomba hata serikali inaomba,cha ajabu ni nini wanachi wake wakiomba....???

sio kosa KUOMBA,ndio njia pekee ya kumjulisha mwenye nacho kwamba huna na unahitaji msaada...unategemea mtu from nowhere aote ndotoni kuwa charity naye anahitaji ticket....???

kama wewe pesa yako ni bora imsaidie mtu yatima good for you,ila kuna wengine ni bora amchukue mtu waende wakastarehe wote!!!ni choice ya mtu at the end of the day!!,jaribu kuwa na mipaka!,usilazimishie what you think, how money should be used...!
 
ri

nikisema uhuru wa mtu na pesa zake,sikuwa namuongelea charity!nimemaanisha...waache hao wanaotaka kumsaidia charity kwenda kuiona hio mechi wafanye hivyo,its their money!!!
 

No wonder nchi yetu iko masikini.Kuna section nzima ya Watanzania inayofikiria kama wewe.Huwezi kufikiria long term, huoni zaidi ya urefu wa pua yako.

Kwa taarifa yako tu, moja ya sababu inayoifanya Tanzania kuwa maskini mpaka leo ni matumizi mabaya ya fedha.Kuanzia serikalini mpaka kwa wananchi kama hivi tunavyoona.

Badala ya serikali kutumia fedha chache za kigeni tulizonazo kuongeza uzalishaji wa uchumi, watu wananunua mishangingi kila mwaka, watu wanatumia mimilioni ya dola kwenda kuleta timu ya Brazil, kwisha hapo mimilioni mingine wanakwiba.

Na wananchi nao wanachangia, wenye kuiba ili kupata kiingilio ndio hao wanakwiba, wenye kuiba ili waonekane mapedejee nao wanakwiba ili kujionyesha kwa visunguratope ombaomba kama kina Charity.

Basi ilimradi kila mtu anataka shortcut, ukiwaambia watu nendeni shule kuongeza ujuzi, mpate elimu ya kujikimu, wanakuona mkali unawakaripia.

Kumbe unawaambia ukweli.

Sasa nchi itaendeleaje wakati damu yake ishaingiwa na hili li UKIMWI la kuomba omba?

Yaani mtu anatumia irresponsible borrowing na fiscal irresponsibility ya serikali kujustify fiscal irresponsibility ya watu.

Two wrongs do not make a right.
 
ri

nikisema uhuru wa mtu na pesa zake,sikuwa namuongelea charity!nimemaanisha...waache hao wanaotaka kumsaidia charity kwenda kuiona hio mechi wafanye hivyo,its their money!!!

Sijamkataza mtu kutoa pesa zake kwa ujinga huu, hili nimeshalisema hapo juu.

Ninaeleza msimamo wangu kuhusu swala hili. Na mimi kama mmoja wa members wa JF, niliombwa msaada, nikatoa majibu yangu ambayo yanajumuisha mtizamo wangu na falsafa yangu ya maisha kuhusiana na kuomba omba.

Katika kueleza msimamo wangu, najikuta napambana na kansa ya kuomba omba katika kila kona.

Kwa hiyo kama nilivyosema mwanzo, Charity ana haki ya kuomba na watu wana haki ya kumpa, indeed hata kama ningekuwa nataka kuwazuia watu wasimpe ningewezaje wakati watu wana ma PM na ma Western Union?

Ninachosema kumpa hela huyu dada ni sawa na kulipa teja la madawa ya kulevya hela ili linunue madawa. Likoverdoze damu yake itakuwa juu yako.

If you fuel this habit and this woman turns completely dependent you will have contributed to that.

Kama vile Charity alivyo na uhuru wa kuweka bango la ombaomba hapa, na watu walivyo na uhuru wa kumpa au kutompa, na mimi nina uhuru wa kushurumu tabia ya kuombaomba bila tija.
 

sikuwezi babu wee....

ngoja nikuache,maana naona sikuelewi na wala sitakuelewa...

kuomba kwa mtu kama charity sijui vina uhusiano gani na matumizi mabaya ya serikali?...

mwaya Charity sina hio pesa...mie ningekupa..:hug:
 
sikuwezi babu wee....

ngoja nikuache,maana naona sikuelewi na wala sitakuelewa...

kuomba kwa mtu kama charity sijui vina uhusiano gani na matumizi mabaya ya serikali?...

mwaya Charity sina hio pesa...mie ningekupa..:hug:

Of course huwezi kunielewa.

Charity na serikali yake wana tabia moja, fiscal irresponsibility na kuishi lifestyle wasiyoweza kui afford. Zaidi ya hapo wote hawana priorities katika maisha haya.

Ndiyo maana viongozi wetu wanajenga mihekalu ya mamilioni ya dola bila aibu, wakati nchi masikini.

Ndiyo maana viongozi wananunua mishangingi kila mwaka, wakati nchi masikini.

Ndiyo maana serikali inatumia mamilioni ya dola kuleta Brazil, wakati kinamama wanakufa kila siku kwa sababu hatuna facilities wodi za wazazi, hatuna vitanda mahospitalini, hatuna madawati mashuleni, matatizo kebekebe muhimu tunayo, lakini tunafuja fedha za umma.

Kufuja huku kwa fedha na mali kunaonekana kuwa si tabia ya wakubwa tu, bali hata baadhi yetu wananchi wa kawaida tunapenda anasa tusizoziweza.Ndiyo matokeo yake mtu hana hela ya kiingilio cha mechi, kitu ambacho si lazima, anakuja kuuza utu wake hapa na kuwa ombaomba ili apate hela ya kuingilia uwanjani.

What is next now?

Ohio St. ?
 
NO si sawa...:angry:

Ni sawa kwa sababu zote mbili ni addictive na destructive habits.

Huyu dada anakuwa addicted na lifestyle asiyoweza kui afford

Teja linakuwa addicted na madawa ya kulevya.

Sooner or later teja litaoverdose, na huyu dada ataendekeza tamaa na kufanya kitu kibaya, ataiba, atasaliti ndoa/penzi kwa ajili ya tamaa.

ku fund any of the two ni ku fund destructive habit.Wenetu waliosoma psychology wanaiita hii tabia "enabling".Tusitake kumu enable huyu teja hapa.
 
Kiranga mkakati ni upi sasa maana tunatakiwa kuandamana au kubeba mabango hapa tafadhali mwenye taarifa zozote tafadhali
 
za nini tukifanye maana hii ishu inatia kichefu chefu mtu aje kucheza na wewe umlipie na chakula na usafiri bado umlipe hela kibao. Isitoshe bado anakuacha na njaa. Kucheza na Brazil ni sawa na kwenda bar kunywa beer halafu ukitoka hapo ukaombe hela ya chakula. Hela zenyewe wala hawatazitumia hapa na matokeo yake kila kukicha shilingi itaendelea kushuka. Ndugu mwana JF tumia muda wako kuelimisha wananchi ili8 waweze kuzitumia kura zao vizuri hatuwahitaji bora viongozi bali tunahitaji viongozi bora na makini.

N.B Hivi kwanini kila uchaguzi unapokaribia mafuta lazima ya pande na kusabababisha vyakula kupanda?
 
Je kama serikali inajali kulikoni kuwapa hawa Brazil kwanini wasifanye kama kenya hela hizi hizi wawe wanatoa motisha walau wa 50000/= kwa mwezi kwa kila mwalimu ambaye anafanya kazi vijijini na hii ingechochochea walimu kwenda kufanya kazi vijijini kuliko kulundikana DSM huoni kama ingesaidia sana kuwainuia kielimu watoto walioko kule vijijini na kuwa na maendeleo baadae kwa taifa letu.

Lakini kwanini hamumuelewi kiranga anachosema hapa why?
 
Kiranga I conquer with you mkuu

Ili Taifa lijikomboe ni Lazima watu waelimishwe umuhimu wa Individual Responsibility kwamba sio eti kwa sababu hata kama nisipoenda mimi wengine wataenda au eti hata kama mimi nisipokipigia kura chama fulani wengine watakipigia basi na mimi nikipigie LoL huo ni Utumwa wa Mawazo na mbaya zaidi

Mkuu Kiranga I admire you sometimes Mungu akuongezee Nguvu uzidi kuchangia JF, JF need critical people like you, You call a spade a SPADE hakuna kumung'unya maneno
 

...ungekuwa na evidence hii sio mara ya kwanza dada charity kuomba,ningekuelewa zaidi,,,

...hizi ni story zako,havina uhusiano na si sawa,unalazimishia ionekane ni sawa mpk unatia aibu...!
 

good,kama umeelewa hilo!!...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…