Harambee: Kuiona Mechi ya Brazil na Taifa stars


Mechi ni June 6, sasa too late inakuwaje?

Mimi naongea na individuals ambao wanafanya maamuzi ya kwenda au kutoenda, sasa utasemaje niko too late?

Kuna watu wanaangalia hii debate kabla hawajanunua tiketi, na debate hii ina wa inform kuhusu wanunue au wasinunue tiketi.Sasa utasemaje niko too late.

Na mtu anayeongelea principle hawezi kuwa too late, principles fulani, kama fiscal responsibility hubakia vile vile, whether event imepita au la.

Na always kuna somo la kujifunza kutoka principles, hata kama event imepita, unaweza kutumia principles hizi kuzuia kurudia incident.

Hapa naona wabongo wanaenda na "mob psychology". Nina hakika hata kwenye uchaguzi watapiga kura hivi hivi na "mob psychology". Nitapigia kura chama fulani kwa sababu nisipopigia jirani yangu atakipigia.

Hatuna personal responsibility.
 
Usijali wewe unataka utoke na nani Kaka au Lucio? Napokea booking zenu.

Hahhaaaaa mpwaz sasa mbona unanitisha kumbe wewe ni agent tena??
mi nlidhani out of kujuana na washikaji wa Brazil ndo uta ni hook up??
 

unafikiri kama watu wote hapa jf hawatenda kwasababu ya kusikia wito wako, uwanja hautajaa? mbona wachache sana wanaenda kuangalia huu mpira hata hapa jf....wengine hawako Dar, wengine hawako tz just a handful of people ndo wataenda...so strategy yako ni mfu/dead...tafuta ingine.
 

Charity nilikuwa mkoa kwenye kugawa neti zilizotolewa na ccm za mpango wa kupambana na malaria kwa watoto chini ya miaka mitano...sasa nimerudi samahani kwa kuchelewa kuona threads yako ila sijachelewa wakati nasoma hii thread amepita mzungu bosi wangu hapa amekupenda kwanza ulivyo natural kuanzia sur na maneno yako! ila yeye sharti ni moja atapenda kwenda na wewe kuangalia hiyo mechi mengine mtakubaliana wenyewe ameuliza eti umeolewa...sijui shonga ndio kashazimika please nijibu....
 
Mimi ningetoa mkwanja wote kabisa (200,000) lakini tiefuefu wamedai tiketi za laki 2 zimeshaisha.....
 

Kiranga,

Ni watu angapi watakao fanya maamuzi yao kupitia kwa maoni yanayotolewa kwenye hii post, kwa hizi siku sita au saba zilizobaki? Katika watazamaji elfu sitini, wangapi wataguswa na maoni haya? Kwahiyo kutoa hamasa ya watu wasusie hii mechi katika thread ya mwenzako, ni kuwa na kimbelembele tu. Anzisha thread ya kwako labda yenye kichwa "Wanajamii wasusie mechi ya Stars na brazil". Kwa taarifa tu ni kuwa, makampuni mengi yameshajitokeza kununua tiketi nyingi kwa ajili ya kuzitoa kwa wadau wao mbalimbali. Hivyo, hiyo mechi itafanyika tu, na uwezekano wa watu kufurika ni mkubwa sana. na hakuna kitu cha Mob psychology hapo.

Pia kumkejeli mwanzisha thread, eti analeta umasikini wake kwenye forum wakati uwezo hana, ni kukosa adabu na ufinyu wa fikra. Kwa mtazamo wako, hata kama kweli unataka kumsaidia kumlipia kiingilio hicho, utampataje huyo Charity?
 

bora umemwelimisha huyu ndugu, manake ni mgumu sana kuelewa. yupo yupo tu maadamu ametoka na post yeye anafikiri yuko juuuuuu,unajua mtu asiyeelewa huwa hajijui kama haelewi..
 

Mumy kuna Pedeshee mmoja wa hapa mjini, maeneo ya Temeke amekubali kukunulia ticket mbili...ila kuna some strings attached to......tumasharti twa kiutu uzima....atakuM nimempa ID yako ya JF....all the best
 

You are missing the point.

Point si uwanja usijae, ni mtu anayekuja na mentality ya "nisipoenda mimi jirani yangu ataenda" ndiye anayeweza kuja na swala la uwanja kujaa.

Hapa tunaongelea kuchukua msimamo wa ku register kwamba hatutaki kushiriki katika upuuzi huu.

Unachosema wewe ni sawa na kusema kwamba, Muislam ambaye anaamini nguruwe ni haram, akisikia kuna karamu ya kula nyama ya nguruwe, aende kula kwa sababu hata asipoenda karamu itajaa watu. Hii thinking ni potofu.Kama wewe ni muislam halisi, hutajali kama karamu ya nguruwe itajaa watu au la, wewe utajali principles zako tu kama muislam.

Vivyo hivyo, hii mechi ni kama karamu ya kula nguruwe, kushiriki katika kitu ambacho mtu yeyote anayepinga matumizi mabaya ya fedha za umma ni haramu bila kujali kwamba wengine wanashiriki au hawashiriki.

Ukienda kuangalia mechi hii huna moral authority ya kuishambulia serikali kwa kuileta Brazil. You cannot eat your cake and have it too.

Either una maintain moral authority kwa kutokwenda kuangalia mechi, na kutoka hapo unaweza kuishambulia serikali.

Au unaungana na serikali katika upuuzi huu, kwa kwenda kuangalia hii mechi, na kupoteza moral authority yote ya kuishambulia serikali katika hili.
 

wewe unatakiwa kubishana peke yako, kwasababu mgumu kuelewa...sipotezi muda tena kukuelewesha.
 

Kwanza hata kama hakutakuwa na mtu hata mmoja atakayefuatilia maoni yangu, bado nitakuwa nishaji express. Na wachunguzi wa miaka ijayo wakija kwenye archives za JF kuchunguza sababu za nchi tajiri kama Tanzania kuwa maskini, wataona kuna mwaka Tanzania iliilipa Brazil kuja kucheza mechi at an astronomical cost, lakini si Watanzania wote walioshabikia upuuzi huo.Kuna wengine walipinga on principles of fiscal responsibility.

Kuhusu mimi kumdhalilisha mtoa maada, anayemdhalilisha kikweli kweli ni wewe unayetaka kum patronize kama mtoto mdogo.Let's call a spade a spade, anataka kuishi beyond her means, na zaidi ya hapo, anataka wenzake waingie gharama za anasa zake zisizo lazima.

This is the short and the long opf it, however you sugar coat it.Tatizo letu wabongo utamaduni wa kuambiana ukweli hatuwezi.

Mtu akisema ukweli mnasema anadhalilisha watu.

Kama huwezi kumudu anasa kwa nini usiishi maiisha yaliyo katika level yako/. Hii ni tamaa.

Unaona sasa Mapedeshee washaanza kuchangamkia offer kwa "masharti ya kikubwa" ?

Halafu nikisema hii lifestyle ina promote Ukimwi naonekana nina stretch mambo.
 
wewe unatakiwa kubishana peke yako, kwasababu mgumu kuelewa...sipotezi muda tena kukuelewesha.

Mgumu wa kuelewa ni wewe ambaye hata huelewi kwamba mtu hawezi "kubishana peke yake".
 
kombe la mbio za mbuzi eeh??kama mtu anayo hio ticket ampe dada charity,kama hauna tafadhali songa mbele...hatuhitaji kusoma mashudu yenu mareeeeeeefu...lol😎
 
Best unatuchangisha halafu wataka kukaa VIP B? Bora ungechangisha 30000 ili ukae njano na kwekundu nibgekuelewa. Anyways ukifikisha 140000 ntafute ntakutumia kwa VodaCom M-Pesa toka hapa Nairobi!
 
kombe la mbio za mbuzi eeh??kama mtu anayo hio ticket ampe dada charity,kama hauna tafadhali songa mbele...hatuhitaji kusoma mashudu yenu mareeeeeeefu...lol😎

Wewe nani mpaka upange sheria hapa JF?

Hebu soma motto hapo juu "JamiiForums, Where We Dare To Talk Openly"

Hiyo inajumuisha kukemea ombaomba, kukemea watu wanaotaka kuishi kwa anasa wasizoziweza, kukemea matumizi mabaya ya hela za umma, na kukemea umangimeza wa kutaka kuwafunga midomo watu wanaotaka kujieleza.

Wewe unatetea uomba omba, unatetea matumizi mabaya ya fedha za umma, unatetea watu wanaotaka kuishi kwa anasa wasizoziweza na unaleta umangimeza wa kutaka kuwafunga midomo members za JF.

Halafu kesho keshokutwa tunakuja kujibaraguza hapo kukemea ufisadi wakati kwenda kwenye hii mechi ni kufanikisha ufisadi.
 

nimeona mara nyingi unapenda mabishano ya kijinga hapa JF,mie hata hunipati kiranga!!jaza mashudu yako ukimaliza tambaa,,,,muda wa kupoteza na wewe hata sinao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…