Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Kijiji cha Muhoji ni moja kati ya vijiji vinne (4) vya Kata ya Bugwema - vingine ni Masinono, Kinyang'erere na Bugwema. Kata hii ina Sekondari moja iitwayo Bugwema ambayo kwa sasa imeelemewa sana kwa sababu hizi:- Kidato cha Kwanza (Form I) cha mwaka huu (2023) kina jumla ya WANAFUNZI 362 walioko kwenye Mikondo 7 ya wanafunzi 50 kwa kila mkondo. Iwapo kila mkondo ungalikuwa wa Wanafunzi 40, Form I hii ingalikuwa na Mikondo 9.
- Walimu 10 tu kwa Sekondari yenye jumla ya Wanafunzi 748.
- Mbali ya mirundikano hiyo kwenye Bugwema Sekondari, bado wanafunzi wa kutoka Kijiji cha Muhoji wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 24-30 kwenda na kurudi kutoka masomoni.
Jumanne, 24.1.2023, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mhe. Prof Sospeter Muhongo ameendesha HARAMBEE ya kuchangia ujenzi wa MUHOJI SEKONDARI.
MICHANGO ILIYOPATIKANA
(i) Wanakijijiji wakiongozwa na Diwani wa Kata, Mhe Clifford Machumu wamechangia:
- Saruji Mifuko 124
- Fedha taslimu, Tsh 305,000
- Nguvukazi - kusomba Mawe, Mchanga na Kokoto.
- Tsh 45,000 kwa kila kaya
- Saruji Mifuko 20
- Jana alishiriki kwenye ufyatuaji wa matofali
- Saruji Mifuko 150
- Ataendelea kuchangia
- Ujenzi wa Vyumba 4 vya Madarasa vyenye Ofisi 2 (katikati) za Walimu na Choo chenye Matundu 8 ukamilike kabla ya 30 Julai 2023
- Muhoji Sekondari ifunguliwe Januari 2024
Mtendaji wa Kijiji (VEO)
Samwel Mourice (0686 557 264, 0769 458 012
ELIMU NI UCHUMI
ELIMU NI MAENDELEO
KARIBU TUCHANGIE UJENZI WA SHULE ZETU
Picha za hapa zinaonesha matukio mbalimbali ya Harambee ya ujenzi wa Muhoji Sekondari ya Kijijini Muhoji, Kata ya Bugwema.
Vilevile, Picha 2 zinamuonesha DC Mhe Dkt Halfan Haule (mwenye shati nyeupe) akishirika kufyatua matofali ya Muhoji Sekondari. Hiyo ilikuwa jana, Jumatatu, 23.1.2023
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumanne, 24.1.2023