Harambee za kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya sekondari za kata - Jimbo la Musoma Vijijini

Harambee za kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya sekondari za kata - Jimbo la Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374.

Jimbo hili lina jumla ya Sekondari 27:
  • Shule 25 za Kata/Serikali
  • Shule 2 za Binafsi (SDA & KATOLIKI)

UPUNGUFU WA MIUNDOMBINU

Tunaendelea na ujenzi na uboreshaji wa miundombimu iliyopungufu kwenye Sekondari zetu za Kata.

Bado kuna mahitaji ya Maabara, Maktaba, Vyumba vya Madarasa, Ofisi za Walimu (Majengo ya Utawala), Vyoo, Nyumba za Walimu, n.k. kwenye Sekondari zetu za Kata.

Vilevile, kuna matatizo ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda masomoni, na mirundikano ya wanafunzi madarasani (wingi wa watoto wanaopaswa kwenda sekondari) - tunalazimika kuongeza idadi ya Sekondari kwenye baadhi ya kata zetu.

Tunashukuru sana Serikali yetu, chini ya uongozi wa Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombimu iliyotajwa hapo juu.

HARAMBEE ZA MBUNGE WA JIMBO

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, ataendesha HARAMBEE MBILI kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye SEKONDARI MBILI.

(1) BWAI SEKONDARI - Hii ni Sekondari mpya na ya pili ya Kata ya Kiriba ambayo imefunguliwa wiki iliyopita. Mategemeo ni kuwa na Wanafunzi 150 wa Kidato cha kwanza (Form I).

Harambee Bwai Sekondari
- Alhamisi, 19.1.2023
- Saa 9 alasiri (15 hrs)

Michango ipelekwe kwa:
- Headmaster (0757 471 516, 0612 409 257)

(2) MUHOJI SEKONDARI - Sekondari hii inajengwa kwenye Kata ya Bugwema yenye vijiji vinne (4), na ambayo ni kubwa (eneo) kuzidi Kata zetu zote.

Hii itakuwa Sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema

Harambee Muhoji Sekondari
- Jumanne, 24.1.2023
- Saa 8 mchana (14 hrs)

Michango ipelekwe kwa:
- Mtendaji wa Kijiji (VEO) - 0686 557 264

MICHANGO inaombwa kutoka kwa Wazaliwa wa Musoma Vijijini na hasa wa kutoka maeneo yenye miradi hiyo, na Wadau wengine wa Maendeleo - KARIBUNI SANA!

index.jpg

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
Tarehe: Jumanne, 17.1.2023
 
Kutoa ni Moyo, kwa Ajiri ya Manufaa ya Watoto Wetu Sasa na Baadae..
 
Ivi elimu bure tunayo ambiwa ipo hapa bongo haianzii kwenye majengo??.
 
Back
Top Bottom