Haramu mwanaume kuuza "chupi" saudi arabia!!

bampami

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2011
Posts
5,699
Reaction score
4,117
Sheria mpya inayowapiga
marufuku wanaume kuuza
nguo za ndani za wanawake
kama vile chupi na sidiria
inaanza kutekelezwa hii leo
nchini Saudi Arabia. Wanaharakati wa kike
katika Ufalme huo wa
kiislamu wanatumai kuwa
agizo hilo lililotolewa na
mfalme Abdulla mwaka wa
2006, utamaliza mfadhaiko ulipo wakati wanawake
wanauziwa nguo zao za
wasaidizi wanaume
madukani. ajira kwa wanawake Hatua hiyo itawapa fursa
adimu zaidi ya wanawake
40,000 kuchukua nafasi za
kazi zitakazoaachwa wazi. Maafisa wa kidini
wasiopendelea mabadiliko
wamepinga vikali hatua hiyo
ya wanawake kufanya kazi
nje ya nyumba zao. Serikali imepanga kupeleka
waangalizi katika vituo vya
biashara kote nchini
kuhakikisha kwamba
wasaidizi wanawake
madukani hawabughudhiwi na maafisa wa polisi wa
kidini.
 
Kila nchi ina nidhamu yake, wewe kinacho kukera nini hapo.

Wewe unatazama upande wako, na wao wanatazama upande wao.
 
yaani kuna nchi wanawake hawaishi maisha kabisa, wana ulimwengu mwingine kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…