Hari siyo shwari ndani ya chuo kikuu teofilo kisanji (teku) -mbeya

Hari siyo shwari ndani ya chuo kikuu teofilo kisanji (teku) -mbeya

zacha

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2009
Posts
1,205
Reaction score
1,880
HALI si Shwari Ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) baada ya Uongozi wa Chama cha Wahadhili wa Chuo hicho (TEKUASA) na wanachama wake kutangaza mgomo wa kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Mitihani ambayo inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu kwa kile walichodai Menejimenti ya Chuo kutotoa majibu ya matatizo yao.
Mgomo huo umetangazwa leo na Kaimu Mwenyekiti wa Tekuasa Amani Simbeye katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho kilichopo Block T kata ya Iyela Jiji na Mkoa wa Mbeya na kuhudhuriwa na zaidi ya Wahadhili 30.
Simbeye amesema kuna mambo mengi na changamoto za elimu inayotolewa Chuoni hapo ambazo Menejimenti ya Chuo inahusika moja kwa moja hivyo kuhatarisha mustakabali wa Elimu Nchini hususani inayotolewa Chuoni hapo ambapo ameongeza kuwa zaidi ya yote ni kukosa ushirikishwaji wa maamuzi yanayohusu Taaluma.
1.JPG
2.JPG
3.JPG
4.JPG
5.JPG
6.JPG
7.JPG
8.JPG
Strength and growth come only through continuous effort and struggle.
Napoleon Hill
 
Samahani mtoa mada! Kuandika 'Hari' badala ya Hali kwenye habari inayohusu TEKU, chuo kinachopika wataalamu wa lugha tangu 2006 ni kukikosea heshima. Rekebisha bwana.
 
Samahani mtoa mada! Kuandika 'Hari' badala ya Hali kwenye habari inayohusu TEKU, chuo kinachopika wataalamu wa lugha tangu 2006 ni kukikosea heshima. Rekebisha bwana.
nadhani umeelewa na samahani kwa usumbufu huu ndugu!
 
Majanga hayo, Mungu atusaidie mwaka huu. Kumbe ndo maana hawa jamaa wanatukazia mitihani hvyo?
Hata hvyo Teku ni chuo kilichojaa ubabe na uonevu wa kila aina. Wanachuowalimchagua rais wanae mtaka ila uongozi ukampiga chini, wakamweka wa kwao.Ila naogopa huo mgomo wao usije ukaathiri maendeleo yetu hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa semester.
 
poleni ndugu zangu wa Teku,at the end everything will be alright,if not then it's not the end.
 
hiki chuo kinaendeshwa kibabe sana,huyu Dr Moses na Pro Kassimoto waondolewe kwani wameshindwa kukiongoza chuo. Chuo hakina demokrasi kwa wanachuo ,wanawachagulia viongozi wanaowataka wao ili walinde maslai yao.
 
vyuo vikuu vinavyomilikiwa na madhehebu ya dini vinatakiwa kuwa mfano kwa vyuo vingine ktk utoaji wa elimu bora lakini vyenyewe ndo vinashiriki ktk kudhoofisha elimu!
 
Back
Top Bottom