MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wakuu,
Yapo mambo hayawezi kupita kirahisi ki JF. Majuzi tumemsikia msanii Linah akilalama kudhalilishwa tena mbele ya public na msanii mwenzake Harmonise lakini ni kama linataka kupita kisanii hivi.
Kwanza hata hili likipita yapo "macho" yameona na ku note huu utomvu wa nidhamu wa ajabu kama tuhuma ni kweli. Najaribu kufikiri hizi tuhuma zingemhusu Diamond! Kuna unafiki lazima tuuvunje ili tusiwe taifa lenye laana za kinafiki.
Majuzi Haji Manara alitupiana maneno na Prisca na ikaleta sokomoko kubwa hadi hashtag kuona mwanamke kaonewa lakini hili linajadiliwa kiudaku na hata wanaomhoji Linah lengo ni habari tu na attention lakini si kujaribu kudhibitisha na kukemea kitu hiki cha ajabu kama ni kweli.
Kwanza, nianze na wamiliki wa hizi kampuni za ulinzi zinazotoa bouncers kwaajili ya ulinzi wa VIPs, How comes mnakubali kutekeleza amri za client zilizo kinyume na mkataba wenu? Mnaagizwa mbebe mtu na mnatii bila kujua matokeo yake? Mtakuja kuwajibika! Narudia tena mtakuja kuwajibika kukubali amri zilizo kinyume na mikataba yenu! Nyie sio chawa wa client bali mna mission za kiulinzi ambazo hata vyombo vya usalama vinajua otherwise mtajitia matatani!
Pia, sehemu za starehe! Hivi mnaweza kukubali mteja wenu kubugudhiwa sababu ya umaarufu wa mtu? Kidimbwi kama kilichotokea mliruhusu bila kutenda haki na kujali sura ya mtu mmechora mstari wa kuwahukumu. Lindeni wateja wenu bila kujali majina. Kama wateja wengine wakiondoka na kuwaachia hayo majina mtafunga business.
Mwisho, Rekodi hazifutiki! Wasanii mjiheshimu! Yapo "macho".