Harmonize a.k.a Kondeboy aja na chakula cha bure

Wabongo kuwaelewa mpaka ujitoe ufahamu
Mungu ambariki.
Ninyi mnaosema kuna Mambo mengi ya kufanya nje na Hilo analotaka kufanya,,kwanini msifanye nyie!??
Kwanini mnataka kumpangia mwenzenu Cha kufanya???
 
Developed Countries kuna mpaka kugawa mishahara bure.
Hoja hapa watu wasiojiweza..
Mungu kamjalia kupata pesa kupitia kwa Mzungu wake sasa alichoona kinafaa afanye
Hapo mengine mbona kila siku wapo wanaofanya?
Hivyo tushukuru kwa hata hiyo.
Hizi mambo za kutwist kila wazo la MTU si sawa.Na anapoishia mwingine anzia hapo
Ni idea nzuri ila kama angeielekeza kwa vituo vya yatima na wajane or wazee ingekuwa poa sana, maana kugawa tu kwa mtu yeyote inaweza kuwafanya watu wawe wavivu kutafuta, wakitegemea Harmonize aptishe msosi.
 
Acha tu agawe chakula
Kuna shirika hapa Tz hugawa pesa na mitaji kwa kaya Masikini je wameisha?Tasafu..
Hata chakula ni muhimu.Wakishakula wataenda kwa wanaogawa mitaji..
Kugawana majukumu.
Idea ya hivyo ukimpa MTU chakula kwa Siku 1 hujasaidia Bali umeongeza tatizo.

Agawe mitaji kwa hao anaowalenga kuwapatia hicho chakula. Ili wafanye kazi kuzalisha na wao kuwa na uhakika wa chakula kila kukicha.
 
Haaaa haaaa kazi IPO kachumbarii
Asisahau muda mzuri awe anatugawia saa tano au sita asubuhi na asisahau kua anatuwekea na kachumbari pembeni Mungu ambariki sisi tutasubiri tu msosi maana tunauhitaji njaa isituuwe
 
kugawa chakula me siafiki.

anagawia watu wa aina gani? na usishangae watu wazima wakawa wanapanga foleni msosi wa bure. bila haya.
Kweli! apeleke kwenye vituo kama vya watoto yatima na wazee, apeleke hata magerezani, mahospitalini na sehemu zingine zenye uhitaji!
 
Mm tayari nafanya nimetoa 75K kwa akina mama 20 kwa kila mmoja hapa mtaani miezi mitatu iliyopita baada ya kuona idea yao ya kufanya kazi ya umama lishe ni nzuri. Sema wengine hatupendi showoff
Mbona yeye hakukupinga? Angesema kwanini unatoa 75K badala yake ungewajengea vibanda vya biashara ungeonaje? Sio showoff kwakuwa hakuna aliyekushuhudia humu kaka.
 
Nampongeza kwa moyo wa kujitolea. Ila Sustainability ndo tatizo na hawezi kumgawia kila mtu chakula. Angekuja na wazo la kuwasiadia watu kupata kipato endelevu na kisha wakajinunulia chakula ingekuwa vyema.
 
kugawa chakula me siafiki.

anagawia watu wa aina gani? na usishangae watu wazima wakawa wanapanga foleni msosi wa bure. bila haya.
Kwa wanaume wa Dar kupanga foleni kwenye chakula cha bure hilo linawezekana kabisa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kuna vitu vingi vya kufanya kuisaidia jamii badala ya free food
Nawewe si ukafanye hivyo vingine? Hivi ni lazima kila mtu afanye vile unavyovipenda wewe? Mi Tanzania bana, shitholes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…