Harmonize acha kutafuta public sympathy.Hii itakugharimu in long run

Acha kulazimisha mawazo yako yawe ya wengi, yaani ampende zaidi, mboso, Hamonise na asimpende kiivyo dada ake? Tunarudi pale pale Diamond anataka wasanii wenye uwezo na hata kuondoka Hamonise linakuzwa kwa sababu ya hofu anaweza kumfunika. Queen Darlin ni msanii wa WCB, kusema hawawekezi ni kujidanganya tu Darlin hana uwezo ndio maana bosi hatumii nguvu nyingi, Konde boy ana uwezo na akiguswa kidogo tu ana sogea hahitaji nguvu nyingi.
 
Yeye anawasapoti wenyewe mikausho mikali!

Aah sio fresh
 
Watanzania tunapenda sana kukuza mambo mkuu, yaani kwa namna nyingine ni wachonganishi sana kama huyu mleta mada.
Kwani harmonize kujitoa wasafi inamaana ameanza nao vita??? Ina maana tayari wale ni maadui?
 
Jamani wabongo....mimi nilipenda abaki WCB lakini sina tatizo na yeye kujitoa hadi ionekane kuwa ametangaza vita. Au mpenzi myplusbee unasemaje
Baby, unajua mashabiki wa Tanzania ni hovyo sana! Na yote hii ni kwa sababu huwa hawamshabikii mtu kutokana na kazi zake bali kwa sababu ya mtu mwingine! Hao ni wale waliokuwa wanamshabikia Harmonize kwa ajili ya Diamond badala ya kumshabikia kwa kazi zake! Na hata hawa wanaomshabikia sasa, wengi wala hawana tofauti na hao waliokuwa wanamshabikia kwa ajili ya Diamond! Yaani ni very stupid! Kwangu mimi, atoke au abaki wala sioni tatizo lakini kama anatoka WCB na kwenda label nyingine basi atakuwa anafanya ujinga kwa sababu huko anaenda kutumika tu! Lakini kama ataanzisha label yake mwenyewe na kuzungukwa na wajuzi wa tasnia ya muziki na sio opportunists, atakuwa amefanya jambo jema kwa sababu nae anaweza kwenda kuzalisha akina Harmonize wengine!
 
Hapo ruby unamshindanisha na Queen Darleen kweli eboooooh?Darleen level nyingine.
 
Una uhakika gani kama kawapa faida?na je kama bado anadaiwa?
 
Harmonize mpaka afikie level ya diamond itamchukua miaka 1000,000,000 ebooooh.
 
Watu mmekalilishwa tu harmonize ametoka pale kwa amani wasafi wenyewe wamesha sema watampa sapoti yoyote atakayotaka hata kufanya kazi nao wakaenda mbali na kusema hata uko yakimshinda anaruhusiwa kurudi nyumbani team zinawafanya watu muwe wajinga
Wapuuzi hao
 
Kwani wewe utaendelea kulala na Kula ugali wa baba na mama hadi unazeeka lazima utoke ukajitegemee.
 
Japo sijakisoma hicho kitabu ila naona kinanikumbusha "vita ya kiuchumi" ya mzee baba[emoji23]
 
Harmonize mpaka afikie level ya diamond itamchukua miaka 1000,000,000 ebooooh.
Nipe moyo tu, Diamond ni beat na jina ndio vina mbeba, lakini kwenye mashairi ni hakuna na ndio maana nyimbo zake zinakumbwa na balaa la kufungiwa, analazimisha vina hata kama anaimba tusi. Ni wakati wake tu hata MR. NICE aliimba KUKU KAPANDA BAISKELI na akapata jina na pesa ndefu ulikuwa ni wakati wake ila sio kwamba alikuwa na nyimbo nzuri kuliko wengine.
 
Kwenye mashairi ww unaangalia nini,vina au mizani?Kama unaangalia hivyo,Diamond kwenye nyimbo zake zote zina vina na mizani,ila yy kaamua kujikita katika BURUDANI kama content yake kibiashara (kwani Mziki kazi yake ni KUBURIDISHA na KUELIMISHA)

Diamond ni mwimbaji ila ana gene za Hip hop ndio maana Diamond ana Flow nzuri upande wa Hip Hop kuliko baadhi ya wasanii wa Hip Hop,sema tu ameamua kuimba sababu anaamini ndipo anajua zaidi.

Kama hujui hamna waandishi wazuri wa mashairi kama wana hip hop na ogopa msanii ambaye zamani alikuwa mchanaji baadae akaamua kuimba,huwaga anakuwaga mzuri sana upande wa uandishi,sababu bado ana zile gene za hip hop.

Mwisho ukipata muda kasikilize Jisachi-Diamond Ft Mabovu,ngweair,Sikiliza Fesh rmx Fid ft Diamond,sikiliza Zigo rmx Ay ft Diamond,sikiliza Godzilla ft Diamond,Mako chali-Mtoto wa Mama.
 
Reactions: Qwy
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…