The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
NYOTA wa Bongo Fleva, Harmonize a.k.a Konde Boy amemuomba msamaha Diamond Platnumz kwa tofauti zilizowahi kutokea kati yao, ikiwamo cha siku ya karibuni wakiwa visiwani Zanzibar.
Kupitia Insta Story yake, Harmonize ameandika kuwa anatumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kuomba msamaha kwa yeyote aliyemkosea, akisisitiza kuwa hana tena nafasi ya kutoelewana na mtu yeyote.
"Naungana na waislam wenzangu kumuomba Mungu msamaha wa makosa yetu tuliyoyafanya kwa kukusudia na kutokusudia bila shaka Mungu ni Mwingi wa kusamehe atatusamehe In Shaa Allah. Kipekee kabisa nimuombe msamaha yeyote niliyemkosea, kwani bado nina sifa za kibinadamu ikiwa ni pamoja na kukosea!!!"
"Kutoka ndani ya moyo wangu kwa dhati kabisa!! Nimemsamehe yeyote tuliyekwazana kwa lolote!! Kupitia mwezi huu mtukufu, nitahakikisha kila changamoto na tofauti zozote nazitatua!! Namuomba Mungu kupitia neema ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ulete mapatano, maridhiano na kazi ziendelee. kila anaye soma maandiko haya anamchango wa aina yake katika maisha yangu!!!! "
Tarehe 15 mwezi huu wa tatu In Shaa Allah natimiza miaka 31, Alhamdulillah namuomba Mungu uhai, afya pamoja na riziki ninayostahili. kipekee kabisa sitaki kuhusishwa au kutajwa katika tofauti zozote zile kwani hazimpendezi mungu, binafsi nimezichoka."
"Safari yangu ya Zanzibar imenivutia, bila shaka imekuwa kama ukumbusho kwangu, kwamba maisha ya upendo ni bora zaidi kwa namna yoyote ile. Sikutakiwa kurushiana maneno na my brother Naseeb, so sorry my brother, i apologize, nilichelewa kutambua hakuna mkamilifu. tuliyofanya pamoja ni mazuri na ni mengi kuliko shetani aliyekati yetu. sioni haja na faida yake!!!!"
"Mwezi mtukufu wa ramadhani huleta amani na upendo kwa watu wote"