Harmonize anafanya nini Marekani?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Kuna kipindi Nilipitia Instagram Niliona Kama Harmonize Anataka Kwenda Marekani Kufanya Tour Kule. Nilijiuliza Vitu vingi sana kuanzania Management aliyonayo, Promoters Anao Watumia na Aina ya Nyimbo alizo nazo na Watu alio washirikisha.

Kuimba Kiswahili na kwenda kuperform Taifa ambalo haliongei kiswahili na kutegemea waswahili kujaza Kwenye Show Yako Ni Kujitafutia Matatizo.

Siku Za Mwanzo Niliona Video za Show Zake Akiwa Anajaza Kiasi cha Kuhamasika kama Mtanzania, Hasa Show aliyopiga Siku Ya Kwanza.

Lakini Kadri siku zinavyokwenda Naona Ni Kama Show zinakuwa Mbovu sanaaaa Kiasi kwamba Naona Aibu mimi, Japo kazi anayo fanya ni kubwa.

Well, Kama Promotor anamlipia Gharama zake za show ambazo ziko Fixed Well and Good Hatapata hasara itabaki kwa alie andaa show, so suala la Harmonize kujaza halitamuhusu. Ila kama Anafanya show then pesa inayopatikana ndio wanagawana Ni Bora Akarudi Tanzania Kuandaa hit Songs zingine Kali au kufanya Show Kubwa Dar Es Salaam au mikoani Kufidia Hasara Anayo endelea Kutengeneza.

Ni Vizuri akachange Return Ticket yake mapema. Kama Video nazomuona Akifanya show ni Zake Basi tuna Safari ndefu na Ngumu sanaaa Kuhusu Muziki Wetu wa BongoFleva.

Inakuwaje Msanii Mkubwa Kama Harmonize Afanyie Show Mlangoni tena palipo Andikwa EXIT? as if Kwenye Show kuna Wahuni ambao Anytime wanaweza kufanya chochote?

Inakuwaje Anaenda Kuimba Nyimbo za Kampeni ya Magufuli Marekani Huku Akiwataja UGANDA NATION?

Kuna Shida Pahala Hasa Kwenye Management ya HARMONIZE, Harmonize ni msanii mkubwa sana Sio wa Kutendewa haya yanayoendelea Marekani.

Niliwahi kusikia Nigeria Kuwa wanacheza saba Nyimbo zake kwanini asiende Huko? Au Somalia, Madagascar na Kwingine?

Jembe Ni Jembe Jitafakari sana Daktari.
 
Mpambe wa diamond kazini......
umeiandika kwa umakini mkubwa
 
Hii nchi imejaa mijitu iliyojaa majungu na roho mbaya.

Muziki wa East Africa bado sana. Kila msanii anaekwenda huko majuu, anaenda kutumbuiza wabongo walioko nje. Kuna wabongo gani wa maana huko nje ??

Kuhusu mameneja, wote hapa bongo hakuna mwenye maajabu.

Wote wanafanana.
 
Nchumali ni real fighter Kwa hlo big credit na salute sana

kule kiringe cha majungu hawapendi kabisa mtu aonueshe nia kufanya kama au zaidi ya wao.

yaani huwa ni vurugu,nimeona jamaa juzi anaunua cheni la mabati kwa $ za kujesabu kwa mikono,anadiss wengine waache kuvaa mabati.

umasiniki ni roho,chafu.
 
Kuna kipindi Nilipitia Instagram Niliona Kama Harmonize Anataka Kwenda Marekani Kufanya Tour Kule. Nilijiuliza Vitu vingi sana kuanzania Management aliyonayo, Promoters Anao Watumia na Aina ya Nyimbo alizo nazo na Watu alio washirikisha.
Wasanii wote wa tz huwa wanaenda marekani kufanya nini???

Heading ingependeza kuwa hivi

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Una makasiriko sana na waliofanikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…