Harmonize kutoka WCB ni ‘kiki’ ama ‘busta’?

Rlechas_3a60

Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
12
Reaction score
27
UKWELI uliowazi huthibitishwa na mpenyo wa uongo kwenye ngoma za masiko ya binadamu aliyehai na utimamu wa fikra zenye utambuzi wa weledi katika jambo husika.

Kuna mambo katika nyakati huleta tafrani kidogo kwa wenye utambuzi wa kina katika ulimwengu huu wa mapinduzi makubwa ya sayansi na teknolojia kwenye karne ya 21 yenye mateso ya pesa kazi na mapenzi.
Kuna nyakati unawaza hivi ni kweli haya maisha bado yanahitaji kisomo cha juu sana kupata ufumbuzi wake? Amini usiamini huwezi kupata jibu moja kwenye fikra za mawazo yako bali yatakuja majibu mengi yanayokutaka kuwaza kwa sauti.
Ngoja tuteme mate masafi kwenye ardhi inayonuka kila upande, iliyojaa malaika wa giza wanaoangaza kulia na kushoto kusaka riziki yao.

Wakati Bongo Fleva inaasisiwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 kulikuwa na makundi mengi sana ya muziki kama Daz Nundaz, TMK Family, Kwanza Unit, Diplomats chini ya Saigoni na Balozi, Gangwe Mob, Mabaga Freshi, Watengwa, Wandago Family, Waswahili chini ya Pengo, Kikosi cha Mizinga, East Coast Team na mengineyo.
Enzi zile makundi hayo yalidumu kwa muda kiasi japo yawezekana hayapo leo, lakini yalijenga umoja kwa sababu ya umaskini wake licha ya baadhi kujiweza kipindi hicho.
Ukijaribu kuwaza kwa sauti kama makundi hayo katika ubora ule yangeanzishwa sasa, wasanii hao wangepiga pesa kiasi gani?

Baada ya makundi hayo kuyumba hapo katikati yaliibuka mengine, lakini hakuna linalopumua kwa pua zake mbili mengi yamepotea na mengine yanapua moja tu.
Picha likabadilika baada ya kuanzishwa kwa Wasafi Classic Baby (WCB), miaka minne iliyopita chini ya Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ ambaye alianza kumsainisha Harmonize, kisha wakafata akina Rayvanny, Lavalava kisha Mbosso.
Kwa miaka minne hii wametikisa mno, licha ya kubebwa na kila aina ya kiki za kujibamba kuendelea kuwaweka kwenye ramani ya kitaifa na kimtaifa kutokana na ngoma zao kubamba sana.

Kila mtu anahitaji kusikia kitu kipya, kila mtu anahitaji kuona jambo jipya hata kama halina maana huwa bora, kwani yaliyobora hayapewi utulivu wa fikra.
Hapa ndipo WCB wanaanza kuwapa mashabiki zao wasichokihitaji wala kukitamani japo kama kikiwa kwa mlengo chanya kitakuwa ni kuzidi kuubusti muziki wetu kama kuna weledi ndani yake.

Habari zinazopenya katika ngoma za masikio ya wengi ni kujiengua kwa Harmonize ndani ya WCB, ikielezwa kuwa hana maelewano na bosi wake Diamond.
Ukweli ni upi kama tutashindwa kuuchanganya na uongo ili kuudhihirisha ukweli wa jambo lenyewe ikiwa wahusika wanaendelea kuwaimbisha mashabiki zao mitandaoni japo wimbo unashindwa kukalilika kwenye vichwa vyao.

Washikaji zangu wanadai kuwa yawezekana kuwa ni ‘kiki’ maana siku za hivi karibuni wababe hao wa ‘kiki Tanzania’ wamepoa sana, wahanahitaji busta ya kuendelea kukaa kwenye midomo ya mashabiki zao.
Hawa binadamu leo hawana shida kama mimi, licha ya kuwa namwaga jasho kama wao naumiza akili, ila ni mashujaa na maarufu kuliko mimi ndio maana nawaanika hawa viumbe ndio wakati wao.

Awali kwenye tasnia ya muziki na filamu baadhi ya wasanii wamekuwa na matumizi sahihi na yasiosahihi ilimradi tu kuziteka fikra za wapenzi na wasio na mapenzi ya kazi zao kutengeneza pesa.

Nani asiyejua Diamond? Hawezi kuishi bila kuzungumzwa mitandao na kwenye vyombo vya habari iwe kwa mazuri ama mabaya.
Bila mitandao ya kijamii machozi ya Vanessa Mdee kuachana na Jux tungeyaona wapi licha ya mafisi kufurahia kutengana kwao watafune mfupa?
WCB wasituumize vichwa maisha yamekuwa tafu sana mjini, kwani huwezi kwenda mjini hujaoga ikiwa mji wenyewe unanuka mbaya.

Hakika maisha yanaenda kasi sana na usipoendana na kasi hii utaendelea kuwa msindikizaji, nchi imechanganya kila mmoja akitumia akili na maarifa ipo siku itakuwa upande wake.
 
Habari za udaku zisizo na faida haina haja ya kuwa ndefu hivi.
 
Hii kama ilikuwa ni KIKI basi itamtafuna sana Harmonize,Mana kuna kitu tayari mashabik wa WCB wameshakijenga vichwan mwao kuwa ana dharau kwa boss wake na mameneja wa WCB.
 
"Washikaji zangu wanadai kuwa yawezekana kuwa ni ‘kiki’ maana siku za hivi karibuni wababe hao wa ‘kiki Tanzania’ wamepoa sana, wahanahitaji busta ya kuendelea kukaa kwenye midomo ya mashabiki zao"

[emoji115][emoji115][emoji115]
Hapo ndipo ulipoharibu uzi wako, WCB hawajawahi kupoa wala kuboa
 
Boya hujui kuandika makelele meengii.. kubaafu[emoji84]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…