Harmonize: Nitagombea Ubunge kutimiza maagizo ya Magufuli

On Duty

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2020
Posts
566
Reaction score
1,083
Wasaalam wana Jf.

Msanii wa muziki bongo fleva almaarufu Kama harmonize ameeleza kuwa atagombea Ubunge kuonesha heshima kwa hayati JPM baada ya kumpa maagizo hayo kabla ya umauti kumfikia.

Msanii huyo ameeleza siku ya leo akihojiwa na wanahabari wa kituo Cha televisheni Cha UTV.

Harmonize amesema.....

Nimeona Ni heshima kubwa sana ambayo mheshimiwa aliyekuwa Rais wa JMT Dr JPM aliyoionesha kwangu kwa kuniambia nafaa kugombea Ubunge,na huu ulikuwa Kama Ni ushauri mzuri kwangu na ninachukulia Kama Ni mzazi wangu kwakuwa alikuwa akitupa ushauri mara kwa mara
 
Pole yake kwa kuchelewa! Yule mzee wa kupitisha majina kibabe hayupo tena! Chama kimesharudi kwa wenyewe. Na ushahidi ni pale tu Dr. Bashiru Ally alipotumbuliwa ndani ya mwezi tu.

CCM ASILI haina huo upuuzi wa kuwapa nafasi watu aina ya huyo Harmonize kugombea Ubunge.
 
Simpendi Harmonize jamani
Spendi muonekano wake,mziki wake,uongeaji wake,scandals zake,uchezaji wake unaboa kinyama!

Harmonize kama utapita hapa tambua kuna member hapa JF hakukubali hata kidogo
 
Simpendi Harmonize jamani
Spendi muonekano wake,mziki wake,uongeaji wake,scandals zake,uchezaji wake unaboa kinyama!

Harmonize kama utapita hapa tambua kuna member hapa JF hakukubali hata kidogo
Binti umeanza kua mganga sasa
 
Anadhani itakuwa Ni rahisi Kama ilivyokuwa kwa mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…