Harmonize; Sitaki kusikia eti wasafi na Diamond ndo wamenitoa kimuziki

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Akiongea na Obinna Tv nchini Kenya amesema huwa anachukia sana anapo ambiwa yeye Ametambulishwa Kimziki na wasafi pamoja Diamond.

"Sitaki Kusikia jina Diamond Wala wasafi kwenye mahojiano yangu, Mimi mwenyewe Kwa Sasa nina Lebo yangu ya konde Gang, niulize kuhusu hilo tu na Mimi mwenyewe, ukiniuliza kuhusu hao nachukia sana tulisha malizana nao na sitaki Kusikia wao ndo walio nitambulisha kwenye mziki". Harmonize akiongea na Obinna Tv ya Kenya.
 
Ni kiki au yupo serious?
 
Shukrani ya Punda mateke...

Kuna watu waliamini Harmonize hajui kuimba, Mond aliona tofauti...

Leo unaleta dhereu?

Fala ni fala tu.
 
Shukrani ya Punda mateke...

Kuna watu waliamini Harmonize hajui kuimba, Mond aliona tofauti...

Leo unaleta dhereu?

Fala ni fala tu.
Nafikiri ukisoma between the line, asingependa kuingizwa strori za label nyingine wakati yeye anatambulisha mambo yake. Kila Mtu anajua wameshamalizana kwa nini kuingiza hizo stori, matokeo yake ni kuhamisha malengo ya interview yenyewe.

Kuna Wamauziki wengi Duniani hukwepa aina hiyo ya maswali kwa sababu mara nyingi hu-divert attention ya kile kilichomleta kwa kutengeneza ugomvi/chuki au mjadala usio wa lazima.
 
Harmonize anaweza kujiona yuko sawa ila ajue kazi ya kukuza kipaji hadi kianze kuleta pesa ni ngumu inayohitaji wito wa moyoni kabisa. Ni watu wachache sana duniani wanaoweza kuvumilia miaka kadhaa kumhudumia mtu hadi kipaji chake kuanza kiingize hela. Itakugharimu muda, nguvu, akili na pesa. Na mbaya zaidi vijana wanaanza kukuzwa kipaji chake akiwa kwenye umri mbaya wa balehe. Kuna muda mtu anageuka baba wa hiari. Ni mengi mno hutokea zaidi ya pesa. Harmonize awe na shukrani.
 
Ukweli hauwezi kuupindisha ,Dayamondi na dabliyusibi ndiyo waliokutoa....hauwezi kubadili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…