Harry Belafonte Miaka 96

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HARRY BELEFONTE MIAKA 96

Miaka ya mwanzoni 1970s nilikuwa napita nje ya ofisi ya British Airways.

Mbele yangu nikawaona Harry Belafonte na Sidney Poitier wanatoka katika ofisi hiyo.

Itaendelea...

Nikawasogelea karibu nikawasalimia na kuomba autograph zao.

Nilikuwa sina karatasi nikatoa kitambulisho changu cha East African Cargo Handling Services wakaweka saini zao nyuma ya kitambulisho changu.

Nakumbuka nyimbo yangu ya kwanza kuisikia ya Harry Belafonte ilikuwa, "Round the Bay of Mexico," ikipigwa katika radio.

Ilikuwa mwaka wa 1957 nakaa Mtaa wa Kiungani Gerezani kwa mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha bint Mohamed.

Jirani yetu kwenye kona ya Mtaa wa Kiungani na Mtaa wa Sikukuu ilikuwa nyumba ya Mashado Plantan.

Hii ilikuwa ndiyo nyumba nzuri kupita zote pale mtaani ikiwa na kila kitu maji, umeme nk.

Namkumbuka mwanae Rita mama yake Mjerumani.

Rita alikuwa mkubwa kwangu kwa umri.

Mashado Plantan alikuwa na mke wa Kijerumani.

Lakini Harry Belafonte alikuwa akipendwa na Bibi yangu Zena bint Farijala.

Bibi kila ilipotokea nafasi ya kuhadithia senema ataeleza movie ya Harry Belafonte "Island in the Sun," aliyoiona na babu yangu Salum Abdallah miaka mingi iliyopita katika ujana wao.

Kipande alichopenda kuhadithia ni Harry Belafonte kupendwa na bint wa Kizungu.

Basi nami nikawa namjua Harry Belafonte na kupenda muziki wake toka utoto wangu.

Katika nyimbo nilizozipenda ilikuwa, "Coconut Woman."

Baadae Harry Belafonte alipokutana na Miriam Makeba wakawa wanaimba pamoja nikapenda sana nyimbo yao, "Train Song."

Hii nyimbo wameimba kwa Kizulu na waliimba nyimbo nyingi kwa Kizulu na Ki-Khosa na kwa hakika utazipenda.

Mwanangu aliniletea biography ya Harry Belafonte "My Song."

Ananambia kwenye duka la vitabu muuzaji alimuuliza kama hicho kitabu atasoma yeye.

"Hiki nampelekea baba yangu yeye anampenda Harry Belafonte."

Belafonte kuna sehemu katika kitabu ilinihuzunisha kidogo kwani hakumsema vizuri Miriam Makeba juu ya hisani kubwa iliyopitika kati yao wakati wa ujana wao wakishirikiana katika muziki.

Makeba anasema hakuna jambo lililokuwa likimpa raha na starehe kama kuwafundisha Wamarekani kuimba nyimbo za Kizulu.

Miaka ikapita nikajikuta niko New York najibanza Manhattan pembeni ya Hudson River.

Wenyeji katika mazungumzo wakanifahamisha kuwa nikivuka mto tu nitafika nyumbani kwa Belafonte.

Bahati mbaya hakuna aliyekuwa anafahamiananae anipeleke kwake.

Harry Belafonte na Sidney Poitier wamefika Tanzania mara mbili na Hamza Aziz alipata kuwaalika nyumbani kwake kwa chakula cha jioni.

Picha hiyo hapo chini Hamza Aziz kulia akiwafahamisha Harry Belafonte na Sidney Poitier kwa Ally Sykes.




 
Mwaka wa 1985 miezi michache kabla Nyerere hajastaafu urais, Belafonte alikuja Tanzania, akampa Nyerere tshirt ya lile kundi maarufu USA for Africa.

Hukumbuki hili bwana Mohamed? Au ziara muhimu zilikuwa hizo za kukutana na kina Hamza!
 
Mwaka wa 1985 miezi michache kabla Nyerere hajastaafu urais, Belafonte alikuja Tanzania, akampa Nyerere tshirt ya lile kundi maarufu USA for Africa.

Hukumbuki hili bwana Mohamed? Au ziara muhimu zilikuwa hizo za kukutana na kina Hamza!
Gagnija,
Sikumbuki hilo.
Nakushukuru kwa kunikumbusha.

Hukupenda mimi kumwandika Hamza Aziz?
 
Mwaka wa 1985 miezi michache kabla Nyerere hajastaafu urais, Belafonte alikuja Tanzania, akampa Nyerere tshirt ya lile kundi maarufu USA for Africa.

Hukumbuki hili bwana Mohamed? Au ziara muhimu zilikuwa hizo za kukutana na kina Hamza!
Sahihi kabisa. Na Harry Belafonte alifika hadi mkoani Shinyanga. Ni kile kipindi cha njaa kubwa iliyotokea Ethiopia na kuua watu wengi na kupelekea project mbili kubwa za matamasha ya muziki yaliyolenga kukusanya fedha ili kuwasaidia wahanga wa njaa. Projects hizo ziliitwa USA for Africa na British Band Aid ambapo tamasha lake lililoitwa Live Aid lilifanyika July, 1985 pale Wembley Stadium.
 
Dogo, kumbe nawe ushazaliwa miaka hiyo? πŸ˜†πŸ˜†
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…