Nina mpenzi wangu na kweli nampenda sana! Ila huwa nakosa raha na hata hamu wakati wa kujamiiana! Yaani anakuw anatoa harufu kali sana uken wakati wa lile tendo! Kiukwel huyu mpenzi wangu ni msafi na huwa anajijali na isingekuwa hvyo ningesema ni uchafu lakini sio! Ni ki2 gani kinachofanya mpaka sehem hzo zitoe harufu kiivyo? Naombeni msaada wadau ili nilinusuru penzi le2 coz kma tatizo litaendelea kuwa vile kuna uwezekano nikatupa kule!...
Pole MKANDAHARI....Nina hakika mpenzi wako atakuwa na ugonjwa unaitwa 'Bacterial Vaginosis (BV)'. Ni ugonjwa ambao unawatokea wanawake weengi tu na nadhani umeshasabisha wanawake weengi kukimbiwa sababu ya hiyo harufu na kuonekana wachafu, au wanawake weengi tu walio na ugonjwa huo kukataa wanaume kwa kuogopa kudhalilika kuotkana na hiyo harufu. Ni ugonjwa ambao umeshasababisha matatizo meengi tu ya kisaikolojia kwa wanawake kutokana na unyanyapaa.
Lakini wala usitie shaka ndugu yangu, ugonjwa huo unatibika tena kirahisi ajabu nawe uendelee kufaidi 'tunda' lako hata ukitaka kulikoleza kwa 'chumvi'!
Kinachotokea ni kwamba...ukeni kuna bacteria wa aina nyingi tu ambao ni wakazi wa huko na mara nyingi hawana madhara, lakini yanapotokea mabadiliko ya kichumvi ukeni, basi wanazaliana kwa wingi na kusababisha BV (hali hii ni sawa sawa kama fungus aina ya candida wanavyoongezeka ukeni kusababisha candidiasis, lakini candida hawatoi harufu). Hii inasababisha muwasho ndani ya uke na kusababisha kutoa maji maji ya kawaida tu ya uke (kama yale ya wakati wa kujamiiana) lakini yakitoa harufu kali, haswa wakati na baada ya kujamiiana!
Nimeona watu wengi wamekushauri umwambie mpenzio awe anaosha sana uke....lakini ukweli ni kuwa, kuosha sana ndio kunafanya tatizo liwe kubwa zaidi, especially kama anaingiza maji ukeni yakiwa na sabuni (medicated or not) au dis-infectant mfano Dettol. Hizi huharibu zaidi balance ya kichumvi ndani ya uke, na hivyo kuwafanya bacteria hao kuzaliana zaidi na kufanya tatizo liwe worse. Aoshe na maji tu ya vugu vugu yasiyo na kitu chochote.
BV inatibika kwa kutumia antibiotics, mara nyingi za cream za kuweka uko ukeni. Dawa hizi ni Metronidazole (Flagyl) vaginal cream, au Clindamycin vaginal cream...vile vile dawa ya kumeza (vidonge) inaitwa Tinidazole.
Ushauri: Unaweza kwenda kumuona daktari wa magonjwa ya wanawake (Gynocologist) kwa ushauri zaidi. Tafadhali usifanye naye tendo la ndoa wakati anapata matibabu, angalau kwa wiki moja. Mwanaume anapofanya tendo la ndoa na mwanamke mwenye BV anapata hao bacteria, japo yeye hapati dalili..lakini atakuwa anaueneza huo ugonjwa kwa wanawake wengine, na hivyo hivyo kwa mwanamke. Kwa hiyo ni muhimu na wewe ukatibiwa kwa dozi nzima ya Tinidazole. Na tafadhali ASIJIINGIZE VIDOLE AKIJIOSHA NA MAJI YALIYO NA SABUNI AU DETTOL.