KUVIMBIWA (CONSTIPATION BLOATING)
Kivimbiwa ni ugonjwa wa tumbo ambao huambatana na upitaji wa haja (kinyesi) kigumu. Wakati mwingine hutokea kutokwenda haja kwa siku nyingi.Watu wanaosumbuliwa na tatizo la kuvimbiwa wanaweza kuwa na maumivu mengi wakati wa kutoa haja kubwa (kinyesi).
Kuvimbiwa kunaambatana na dalili nyingine za magonjwa ya tumbo.Kuvimbiwa kuna weza kutibiwa kwa njia za asili. Mgonjwa anaweza akawa na uzito katika tumbo.Kuna kuwa na maumivu kutokana na mkuanyiko wa uchafu. Mgonjwa huhisi kutokuridhika. Mtu anaesumbuliwa na kuvimbiwa anaweza kuwa na dalili nyingine vile vile.
Kuna dawa nyingi za nyumbani zitumikazo kwa mtu aliyevimbiwa ambazo zinaweza kumsaidia kupata nafuu kwa njia za asili.Wakati mwingine mtu mwenye kuvimbiwa sugu (mwenye tatizo la kuvimbiwa ambalo linamsumbua kwa mda mrefu) anaweza kuchukua msaada wa kwenda haja ambao husababisha madhara kwa upande mwingine.
Kuvimbiwa ni ugonjwa wa tumbo na huweza kuzalishwa na ugonjwa fulani kama vile kansa ya tumbo. Watu ambao hawali vyakula vya nyuzi nyuzi katika milo yao pia wa athiriwa na ugonjwa wa kuvimbiwa. Unywaji wa kiwango kidogo cha maji pia huambatana na kuvimbiwa. Watu ambao wako katika mazingira ya unywaji wa kiwango kidogo cha maji ni lazima wanywe maji ya kutosha kupata nafuu kutokana na kuvimbiwa.
Watu wengi wanathiriwa na kuvimbiwa kwa sababu hawafanyi mazoezi ya mwili ya aina yoyote. Maisha ya kukaa tu ni sababu nyingine ya kuvimbiwa.Hii huwa kawaida kwa kipindi cha ujauzito. Wanawake wajawazito huathiriwa na kuvimbiwa kwa sababu ya upungufu wa virutubisho katika mlo. Watu huathiriwa na kuvimbiwa hujaribu misaada mbalimbali kwa kujaribu kuondoa tatizo la kuvimbiwa lakin hawapati nafuu.Ni tatizo la mara kwa mara kama mtu hatofanya mabadiliko yoyote katika mlo wake na mfumo wa maisha kwa ujumla.
Ni rahisi sana kuondokana na kuvimbiwa kwa kufanya mabadiliko katika mlo na mfumo wa maisha.
DALILI ZA KUVIMBIWA
Kuvimbiwa kwenyewe ni dalili ya magonjwa mengine ya tumbo na labda huambatanishwa na dalili nyingine vile vile baadhi ya dalili za kawaida za kuvimbiwa ni;
- Ugumu wakati kujisaidia(haja kubwa). Mgonjwa huwa na maumivu makali wakati wa kwenda haja kubwa. Kinyesi huwa kigumu na hufanana na kinyesi cha kondoo
- Maumivu na uvimbe katika tumbo
- Watu wanaoathiriwa na kuvimbiwa sugu wanaweza kuwa na kichefuchefu,kuharisha na kuwashwa
Kuvimbiwa huweza kusababisha matatizo kama kuchanganyikiwa, maumivu ya nyuma ya mgongo, kuumwa kichwa n.k
Ni lazima kutibu tatizo la kuvimbiwa kwa njia za asili kwa hiyi mmoa anaweza akahisi furaha na kupata(haja) na msaada salama kutokana na kuvimbiwa.
DAWA ZA NYUMBANI KWA TATIZO LA KUVIMBIWA
Kuna dawa nyingi za nyumbani zenye uwezo wa kuondoa tatizo la kuvimbiwa kwa haraka.
Dawa hizi za nyumbani zitakusaidia kupata matokeo ya kudumu pasipo kusababisha madhara yoyote yale;
Chukua glasi ya maji weka juisi ya limao pamoja na chumvi kidogo ndani yake. Kunywa mchanganyiko wa vitu hivyo kila siku asubuhi baada ya kuamka kutoka kitandani. Hii ni dawa ya nyumbani yenye nguvu ya kuondoa tatizo la kuvimbiwa.
Inaaminika kwamba mapera ni matunda yanayoondoa tatizo la kuvimbiwa. Kula pera moja kila siku kwa kuondokana na tatizo laa kuvimbiwa .Pera husaidia kuzalisha uteute na kuruhusu kinyesi kupita kwa urahisi kwenye sehemu ya haja kubwa.
Mbegu za flax seed pia hujulikana kwa kusaidia sana katika matibabu ya kuvimbiwa .Chukua kijiko kimoja pamoja na glasi ya maji ya uvuguvugu kila iku asubuhi kwa kuondokana na tatizo sugu la kuvimbiwa.
Chukua majani ya basil na manana na yachemshe pamoja. Kunywa mchanganyiko huo kila siku asubuhi kwa ufanyaji kazi wakawaida wa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
DAWA ZA MITISHAMBA KATIKA PAKITI YAKUTIBU KUVIMBIWA
CHOORNA; ni moja kati ya dawa bora ya mitishamba kwa kutibu kuvimbiwa.Imeandaliwa kutoka katika mimea ya kiasili na imegundulika kuwa ni dawa ya mitishamba yenye ufanisi mkubwa kutibu tatizo la kuvimbiwa. Imeaidia katika matibabu ya kuvimbiwa kwa urahisi na ufanisi. Huzalisha matokeo ya mda mrefu itumikapo kwa utaratibu.
TRIPHALA CHURNA: Divya Triphala churna ni mkusanyiko wa mitishamba mitatu ya kipekee ambayo imegundulika kuwa ni fanisi mno.Katika matibu ya aina yoyote ya ugonjwa wa tumbo.
Mkusanyiko huu wa mitishamba tofauti tofauti ni tiba asili bora sana kwa matibabu ya kuvimbwa na matatizo mengine yanayoambatana na dalili hiyo.
-UDARA-KALPA CHURNA : hii pia imeandaliwa kutoka kwenye mitishamba itumikayo na ambayo ni fanisi kwa matibabu ya kuvimbiwa na dalili nyingine ziambatanazo na kuvimbiwa. Hii ni dawa ya asili ambayo husaidia utoaji rahisi wa haja kubwa(kinyesi).
LISHE INAYOSHAURIWA KWA WAATHIRIKA WA KUVIMBIWA
Ulaji wa vyakula vyenye nyuzi nyuzi kwa wingi, ni tiba nzuri ukiwa nyumbani kupata kuondoa tatizo la kuvimbiwa. Mtu anayesumbuliwa na kuvimbiwa lazima ale zaidi vyakula vya nyuzi nyuzi kuondokana na tatizo.
Ulaji wa mboga mboga na matunda pia husaidia kupata matokeo mazuri kutoka kwenye dalili za kuvimbiwa. Matunda kama vile machungwa, tufaa ni mazuri kwa kukusanya nyuzi nyuzi ndani yake.Pia spinachi,kabichi, nyanya pia husaidia kuondokana na kuvimbiwa.
Supu ya mboga mboga na huandaliwa na kunyewa kila siku kwa matokeo ya haraka ya kuondoa kuvimbiwa.
Unywaji wa glasi moja ya maziwa ya uvugu vugu usiku kabla ya kwenda kulala pia ni njia fanisi ya kuondokana na tatizo la kuvimbiwa.
Lazima kufanya mazoezi kuweka mwili imara na wenye afya. Mazoezi ya mara kwa mara husaidia kujikinga na magonjwa mengine. Matembezi ya aubuhi ni zoezi rahisi ambalo huasidia katika matibabu ya kuvimbiwa sugu.
Epuka kula vyakula vilivyo fanyiwa mchakato(vya viwandani) na vyakula vilivyo na maida. Huweza kuzalisha ukavu katika utumbo mwembamba na huweza kusababisha dalili za mara kwa mara za kuvimbiwa.